AWATAKA VIONGOZI NA WALIMU KUTUNZA MADAWATI HAYO

Mbunge wa jimbo la mkuranga Abdallah Ulega amekabidhi madawati 537 kwa halmashauri ya wilaya hiyo, huku akiwataka viongozi wakiwamo madiwani wa kata mbalimbali kusimamia vizuri madawati hayo ili kutambua mchango mkubwa wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi alisema kuwa madawati hayo yametokana na fedha zao ambazo zilibaki baada ya kubana matumizi katika ofisi ya bunge na kwa kauli moja walikubali kumkabidhi Rais Dkt. Magufuli, ambapo naye kwa kutambua changamoto ya madawati akaelekeza fedha hizo zipelekwe kutengeneza madawati hayo.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Msham Munde alimshukuru Mbunge huyo na kudai kuwa uchangiaji wa madawati hayo ni mchakato endelevu hivyo wadau waendelee kujitokeza kuchangia huku akisisitiza kwamba kwa asilimia kubwa yamekwenda kutatua kero hiyo.

Wakati huohuo mdau wa maendeleo Hamisi Njomoke alimkabidhi mbunge wa jimbo hilo Ulega Madawati 50 kama sehemu ya kumuunga mkono mbunge paoja na Rais Dkt Magufuli huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kuchangia ili watoto wasome katika mazingira rafiki. 
Mbunge Abdallah Ulega akikabidhi madawati 537 kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mkuranga Msham Munde ,madawati hayo yametokana na fedha zilizotolewa na bunge baada ya kubana matumizi na kukabidhiwa Rais Dkt John Magufuli ambaye naye aliagiza zitengeneze madawati.
Mdau wa maendeleo kutoka kampuni ya Hamisi Njomoke Limited akimkabidhi madawati 50 mbunge wa jimbo hilo Abdallah Ulega ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kauli mbiu ya rais ya kuwataka watanzania kujitokeza kuchangia ili kuondoa kero hiyo katika shule leo mokani Pwani.
Mbunge Abdallah Ulega (katika alie simama) akiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya mkuranga Msham Munde, mkuu wa wilaya hiyo Filberto Sanga, na mdau wa maendeleo Hamisi Njomoke mara baada ya kukabidhi madawati 537 ya mbunge wilayani humo.Sehemu ya madawati ya hayo. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii) .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...