Kwa wapenzi na wakereketwa wa burudani ya mchezo wa gozi la ng'ombe yaani kandanda,leo watapata burudani ya aina yake kutoka Sweden na Marekani pale timu 6 zitakapo teremka dimbani kupambana katika mfululizo wa michuano ya kirafiki ya kimatifa (ICC) .

Jijini Stockholm huko Sweden mabingwa wa ligi kuu ya Hispania (LALIGA), FC Barcelona watapambana na mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza (EPL), Leicester City, mchezo ambao wachambuzi na wafuatiliaji wa maswala ya kabumbu wanasema kuwa Leicester City kumfunga Barcelona ni sawa na David kumpiga Goliath.
Barcelona ambao kwenye mchezo wao wa kwanza waliizamisha klabu bingwa ya Uskochi Celtic kwa mabao 3-1, huku ikiwatumia wachezaji wengi wa kikosi cha pili (timu B) wataweza kuendeleza ubabe wao kwa kuzingatia upana wa kikosi walicho nacho. Kwa upande wa Leicester City ambao wao katika mchezo wao kwanza walivulumishwa mabao 4-0 kutoka PSG,watakuwa na kazi ya ziada kuweza kupambana na kupata ushindi dhidi dhidi ya Barcelona.

Nako huko Marekani kwenye jimbo la New Jersey jijini Rutherford ndani ya dimba la Met Life Stadium mabingwa wa Bundesliga,ligi kuu ya Ujerumani, watapambana na vijana kutoka Hispania, Real Madrid ambao ni mabingwa wa Uefa.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na vikosi vyote kusheheni wachezaji mahiri ndani ya dimba,Timu zote hizi zimecheza michezo miwili miwili zikiwa zimepoteza mchezo mmoja na kushinda mchezo mmoja. FC Bayern wao walifungwa na AC Milan ya Itali kwa mikwaju ya penati baada ya sare ya mabao 3-3 ndani ya dakika 90, kisha kuifunga timu ya Chelsea. Madrid wao walinza kwa kupoteza dhidi ya PSG,na kuifunga Chelsea mabao 3-2.
Kocha wa Bayern Munich Carlo Ancelotti ambaye aliwahi kuifundisha Real Madrid amesema kuwa anajivunia zaidi mchanganyiko wa damu changa na kongwe katika kikosi chake, hvyo anategemea kupata ushindi.

Kama hiyo haitoshi ndani ya jimbo la Minneapolis katika uwanja wa Us Bank Stadium,timu ambazo hazikufanya vizuri kwenye ligi zao,AC Milani kutoka (SERIE A) ligi kuu ya Italia na Chelsea (EPL) ligi kuu ya Uingereza, zinapambana katika mfululizo wa michuano hiyo ya ICC.

Katika michezo yao ya awali Chelsea iliifunga Liverpool bao 1-0 na baadaye kufungwa na Real Madrid mabao 3-2 wakati AC Milan waliifunga Bayern Munich kwa penati,kisha kupata kichapo cha mabao 2-0 toka kwa majogoo wa jiji,Liverpool. Kocha mpya wa Chelsea Antonio Conte anategemewa kutumumia uzoefu wake wa ligi ya Italia na kuifahamu vilivyo timu ya AC Milan kuweza kuisambalatisha timu hiyo.

Utamu wa michuano hii unategemewa kumalizika siku ya tarehe 8/8/2016 kwenye dimba la Wembely,jijini London kati ya Liverpool na Barcelona.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...