Mfanyabiashara wa mjini Kahama Mkoa wa Shinyanga, Joseph Machenja amekabidhi madawati 60 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani humo na kuwataka wananchi wote kumuunga mkono Rais John Magufuli katika kutekeleza zoezi hilo.

Akikabidhi madawati hayo kwa Mkuu wa wilaya hiyo Nyabaganga Taraba, Machenja alitoa mwito kwa wananchi kushirikiana na kuendelea kutengeneza madawati ili kuondoa kabisa uhaba.

Alisema zoezi hilo ni endelevu na ndiyo maana ameonesha uzalendo kwa kuguswa na agizo la Rais la kuchangia madawati hayo katika wilaya hiyo japo anatoka Wilaya ya Kahama.

“Nimeguswa na ndiyo maana nimechangia madawati haya ingawa sina mtoto anayesoma katika shule ya Kishapu na pia si lazima uwe mkazi wa hapa, hivyo nawaomba wananchi wachangie madawati,” alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya, Taraba alimshukuru kwa mchango wake ambapo alisema ni moyo wa kuigwa kwa wananchi wengine wa Kishapu japo anatoaka mbali.

Aidha, aliwaomba wananchi wa wilaya hiyo kwa moyo wote waendelee kuchangia madawati kwani zimebaki siku chache kukamilisha zoezi hilo muhimu.

Aliagiza madawati hayo yaende katika shule ya msingi Buduhe na kumkabidhi Mtendaji wa Kata ya Kishapu iliyopo shule hiyo, ambapo alisema yatasaidia wanafunzi 180.
Sehemu ya madawati yaliyotolewa na mfanyabishara Joseph Machenja kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kama sehemu ya mchango wake katika kutekeleza agizo la Rais John Magufuli.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Stephen Magoiga pamoja na mfanyabiashara aliyechangia madawati, Joseph Machenja katika viwanja vya ofisi ya halmashauri.
Sehemu ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakifutahia jambo wakati wa hafla fupi ya kupokea madawati katika viwanja vya ofisi ya halmashauri leo.
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Jumanne Chaula (kushoto) akimshukuru mfanyabiashara, Joseph Machenja baada ya kutoa msaada wa madawati katika halmashauri hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...