Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Benga’i Issa wa kwanza kulia akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu maonesho ya wajasiriamali yataofanyika 
Agosti  26 mwaka huu jijini Dar es salaam , kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji waTaasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Bw. Godfrey Simbeye.



Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Bw. Godfrey Simbeye kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu maonesho ya wajasiriamali yataofanyika S
Agosti  26
 mwaka huu jijini Dar es salaam, kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Benga’i Issa.


Habari/Picha Na Ally Daud. 

Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama anatarajiwa kufungua maonesho ya wajasiliamali yatofanyika Agosti  26 katika viwanja vya Mlimani City ambayo yameandaliwa na Taasisi ya Ujasiriamali na ushindani Tanzania(TEEC) kwa kushirikiana na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ili kukuza uchumi wa nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa NEEC Bi. Beng’i Issa amesema kuwa maonesho hayo yatalenga kuwawezesha wananchi kuwa wabunifu katika sekta ya biashara ili kupiga hatua kufikia uchumi wa kati.

“Maonesho ambayo yatafanyika kesho ni kwa ajili ya wajasiriamali wote wakubwa, wa kati na wadogo ili kuwawezesha kiujuzi na kiushindani katika soko la biashara” alisema Bi. Issa.

Aidha Bi. Issa amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na kliniki ya biashara kwa watu wote kutoka kwa wataalamu wa biashara ili kuweza kuwapatia mafunzo wajasiriamali wakubwa na wadogo ili waweze kupata mafanikio yao na jamii kwa ujumla kupitia biashara zao.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Bw. Godfrey Simbeye amesema kuwa maonesho hayo yatawajengea wajasiriamali fursa za masoko kwa biashara nchini na Afrika kwa ujumla.

“Kupitia maonesho hayo wajasiriamali watapata fursa ya kutengeneza masoko ya biashara zao kwa ubora zaidi nchini na afrika kwa ujumla ili waweze kujitangaza kimataifa” alisema Bw. Simbeye.

Aidha Bw. Simbeye amesema kuwa wana mpango wa kuwaelimisha wajasiriamali kwa wingi zaidi ili waweze kuwa wabunifu na kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya biashara ndani na nje ya Tanzania.

Mbali na hayo Mkurugenzi Simbeye amesema kuwa anawakaribisha watu wote wajasiriamali wakubwa na wadogo kufika katika maonesho hayo ambayo hayana kiingilio ili waweze kupata ujuzi wa kutosha kwa maendeleo ya biashara zao na kuinua uchumi wa nchi.

Aidha Bw. Simbeye amesema kuwa

Taasisi ya Ujasiriamali na ushindani Tanzania(TEEC) itazinduliwa rasmi Agosti 27 na
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...