Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuzindua Mkakati wa Baraza wa Kukabiliana na Ajali za Barabarani nchini. Mkakati huo wa miezi Sita ambao unalenga kukabiliana na ajali umenza mwezi huu Agosti na unatarajiwa kumalizika mwezi Februari 2017 ambapo tathmini itatolewa. Baadhi ya mambo yaliyolengwa katika mkakati huo ni pamoja na udhibiti wa madereva walevi na kuendesha kwa uzembe, udhibiti wa mwendokasi kwa madereva na wamiliki wa magari pamoja na kuanza utaratibu wa Mfumo Nukta (point system) kwenye leseni za udereva ambapo dereva akifanya makosa kadhaa atanyang’anywa leseni na kutokuruhusiwa kuendesha gari tena.  Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuzindua Mkakati wa Baraza wa Kukabiliana na Ajali za Barabarani nchini. Mkakati huo wa miezi Sita ambao unalenga kukabiliana na ajali umenza mwezi huu Agosti na unatarajiwa kumalizika mwezi Februari 2017 ambapo tathmini itatolewa. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kamanda Mohammed Mpinga. Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Na Jonas Kamaleki, MAELEZO
Serikali yajipanga kupunguza ajali za barabarani kwa kiwango cha takribani asilimia 10 hapa nchini ili kupunguza vifo na majeruhi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Yusuf Hamad Masauni  kuwa baraza la Usalama Barbarani linakaerwa sana na kadhia ya ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara.

“Kukithiri kwa ajali za barabarani kwa siku za hivi karibuni, umewezesha Baraza kuibuka na Mkakati wa Miezi Sita (6) unaolenga katika kukabiliana na ajali za barabarani nchini, mkakati huu ni wa muda mfupi kuanzia mwezi Agosti, 2016  had Februari 2017 tutakapokaa na kutathmini matokeo yake”, alisema Masauni.

Masauni amesema ajali za barabarani zimewaacha watoto wakiwa yatima  na kuwafanya akina mamam kuwa wajane, hivyo  juhudi za makusudi inabidi zifanywe ili kupunguza kama sio kuondoa kabisa ajali hizo.

Ametaja vyanzo vikuu vya ajali za barabarani nchini kuwa ni pamoja na Makosa ya Kibinadamu, mazingira ya barabara na ubovu wa vyombo vya moto.
Naibu waziri huyo amesema takwimu za ajali barabarani katika miaka mitatu tangu 2012 ajali ziliongezeka toka 23,578 hadi 23, 842 kwa mwaka 2013, vifo vilikuwa 3,969 kwa mwaka huo hadi kufikia 1,043 mwaka 2013. 

Vifo hivyo vilipungua hadi kufikia 3,760 mwaka 2014, upungufu huo ulitokana na usimamiaji madhubuti wa Sheria na kanuni za Usalama barabarani pamoja na juhudi zilizofanya na Baraza kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Kwa mujibu wa Masauni, Mkakati uliozinduliwa unalenga katika kudhibiti makosa yanayosababisha madhara makubwa na ambayo husababisha kuongezeka kwa ajali za barabarani.

Ameyataja mambo hayo kuwa udhibiti wa madereva walevi na kuendesha kwa uzembe, mwendokasi kwa madereva na wamiliki wa magari, uendeshaji magari bila sifa au leseni za udereva na Bima.

Masauni  ametaja mambo mengine katika Mkakati huu kuwa ni kudhibiti usafirisha wa abiria kwa kutumia magari yasiyo na sifa kama vile Noaha na Probox, ajali za pikipiki za magurudumu mawili (bodabaoda) na matatu (bajaj) na kuhakikisha abiria wanafunga mikanda ya usalama wanapotumia vyomo vya moto kwa ajili ya usafiri.

Maeneo mengine yatakayoangaliwa kwa mujibu wa Masauni ni kuyabaini na kuyadhibiti maeneo tete na hatarishi ya ajali za barabarani (Black spots/kilometres), kuangalia uwezekano wa kufanya marekebisho ya Sheria za Usalama barabarani, kuanza utaratibu wa Mfumo wa Nukta (point system) kwenye leseni za udereva, kutoa mafunzo msasa kwa askari wa usalama barabarani na kutoa elimu na mafunzo kwa bodaboda.


Ili kupunguza ajali za usalama barabarani, Masauni amasema Mkakati utadhibiti vitendo vya rushwa ambapo watoaji na wapokea rushwa wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria, kuwapa tuzo askari wanaofanya vizuri kuzuia ajali na kuwahusisha wamiliki wa magari ya abiria nay a mizigo, katika kuutekeleza mkakakti. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...