THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MHE. UMMY MWALIMU AMUAGA MWAKILISHI MKAZI WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LINALOSHUGHULIKIA IDADI YA WATU DUNIANI (UNFPA) LEO JIJINI DAR ES SALAAM.


Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) anayetarajia kuondoka nchini hivi karibuni Dk. Natalia Kanem (wa pili kutoka kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) mara baada ya kufika Ofisini kwake kumuaga leo jijini Dar es salaam.Wengine alioambatana nao ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) na Dk. Hashina Begum, Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa UNFPA (kushoto).
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) akimweleza jambo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (Mb.) kuhusu machapisho mbalimbali ya Umoja yanayoelezea Maendeleo ya Tanzania leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Dk. Natalia Kanem anayetarajia kuondoka nchini hivi karibuni mara baada ya kumaliza muda wa uwakilishi wa Shirika hilo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (Mb.)akiangalia moja ya chapisho la lenye Mipango ya Umoja wa Mataifa mwaka 2016 -2021 alilokabidhiwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (katikati) , Mwakilishi Mkazi wa UNFPA anayemaliza muda wake hapa nchini Dk. Natalia Kanem (wa pili kutoka kushoto), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez (kulia) na Dk. Hashina Begum, Mwakilishi Mkazi Msaidizi wa UNFPA (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja huku wakionesha chapisho la lenye Mipango ya Umoja wa Mataifa mwaka 2016 -2021 leo jijini Dar es salaam. Picha/Aron Msigwa –MAELEZO.


Na. Mwandishi Wetu - Dar es salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (Mb.) amemuaga Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) Dk. Natalia Kanem anayetarajia kuondoka nchini hivi karibuni mara baada ya kumaliza muda wa uwakilishi wa Shirika hilo. 


Akizungumza na mwakilishi huyo Ofisini kwake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy ameeleza kuwa Serikali itaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Sera, miongozo na sheria mbalimbali zinazohusu usawa wa jinsia na haki za watoto hususan watoto wa Kike.

Amesema Serikali itaendelea kufanya kazi na kushirikiana na UNFPA pamoja na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya Tanzania.

Ameleza kuwa wizara yake itaendelea kuhakikisha kuwa tatizo la ukatili dhidi ya watoto linalohusisha ndoa na mimba za utotoni, ubakaji na ulawiti kwa watoto linamalizika katika jamii ya watanzania

Aidha,amesema kuwa wizara yake itaendelea na juhudi za kupunguza vifo vya mama wajawazito kwa kuweka miundombinu na mazingira bora ya kujifungulia huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuelimisha na kuhamasisha umma wa watanzania juu ya umuhimu wa kuzingatia uzazi wa mpango.

Kwa upande wake Dk. Natalia Kanem ambaye alikua ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano iliyompatia katika kipindi chote alichokuwa hapa nchini na kuahidi kuendeleza kudumisha mashirikiano hayo atakapokuwa Makao Makuu ya Shirika hilo.