Waziri
wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama
ameitaka Mifuko ya Hifadhi za jamii kuwekeza kwenye viwanda ili
kuchochea uchumi wa viwanda utakaolisaidia taifa kukua kiuchumi na pia
kuwanufaisha wanachama wa mifuko hiyo kutokana na uwekezaji huo wenye
tija.
Jenista
Amesema hayo akizungumza na Wakurugenzi wa Mifuko pamoja na Watendaji
katika mafunzo kwa bodi za udhamini za mifuko ya hifadhi ya jamii kuhusu
uendeshaji na usimamizi wa mifuko ya hifadhi yaliyoandaliwa na
Shirikisho la Mifuko ya hifadhi ya jamii (ISSA) .
Amewataka Wakurugenzi hao kuunga mkono Agenda ya taifa ya kulifikisha taifa kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda.
Waziri
huyo amewataka Wakurugenzi wa mifuko kuhakikisha kuwa wanadhibiti
mifuko hiyo ili wanachama waweze kupata mafao yao kwa wakati muafaka
bila kuwepo kwa ucheleweshaji.
Mwenyekiti
wa Shirikisho la Mifuko ya hifadhi (ISSA) Eliud Sanga amesema kuwa
Shirikisho hilo litaendelea kuhimiza Mifuko hiyo kutimiza wajibu wake
katika kutoa mafao bora kwa wanachama wao pamoja na kubuni mafao mapya
ili kuwavutia wanachama.
Sanga
amesema kuwa kwa sasa mifuko hiyo imefungua milango yake wazi kuwapokea
wanachama kutoka sekta ambazo si rasmi ili nao waweze kunufaika na
mafao .
Na Pamela Mollel,Arusha.
Waziri
wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama
akizungumza na Wakurugenzi na Watendaji wa Mifuko ya Hifadhi za Jamii
katika mafunzo yaliyohusu uendeshaji na usimamizi wa mifuko hiyo
yaliyoandaliwa na Shirikisho la Mifuko ya hifadhi ya jamii (TSSA), jana
jijini Arusha.
Mwenyekiti
wa Shirikisho la Mifuko ya hifadhi (TSSA), Eliud Sanga akifafanunua
jambo katika mafunzo kwa bodi za udhamini za mifuko ya hifadhi za jamii
kuhusu uendeshaji na usimamizi wa mifukohhiyo.
Waziri
wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama
akikabidhi cheti kwa Mjumbe wa Bodi ya PPF kutoka TUCTA, Adelgunda
Michel aliyeshiriki katika mafunzo kwa bodi za udhamini za mifuko ya
hifadhi za jamii kuhusu uendeshaji na usimamizi wa mifuko ya hifadhi
yaliyoandaliwa na Shirikisho la Mifuko ya hifadhi ya jamii (TSSA), jana
jijini Arusha.
Katibu
wa Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA), Meshach
Bandawe akizungumza katika mafunzo kwa bodi za Udhamini za Mifuko ya
hifadhi za Jamii kuhusu
uendeshaji na usimamizi wa mifuko hiyo, yaliyoandaliwa na Shirikisho
hilo, jana jijini Arusha.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio akisikiliza jambo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyorara.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...