THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MKALI WA SINGELI KUSAKWA JIJINI DAR


Katikati ni Mratibu wa mashindano hayo Masudi Kandoro kutoka kampuni ya High Time Marketing and Promotion ambao ndio waandaaji wakuu wa shindano hayo amkzumgumza na wanahabari mapema leo wakati wa kutangaza Shindano hilo.(PICHA NA EXAUD MTEI) 

Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania na katika Historia ya music hatimaye mashiundano ya kwanza ya kumtafuta mwanamuziki na mwimbaji wa muziki wa singeli yamezinduliwa nchini, mashindano hayo yakilenga kumpata msanii mwenye uwezo wa kuimba kisingeli mashindano ambayo yamepewa jina la STAR WA SINGELI.

Mashindano hayo yanalenga kuibua vijana wenye vipaji vya hali ya juu ambao wako mitaani nia ikiwa ni kuwainua na kuwafanya kuwa wanamuziki watakaotambulika ndani na nje ya Tanzania huku pia ikiwa ni njia moja wapo ya kutengeneza ajira zenye staha kwa vijana wa Dar es salaam.Akizungumza na wanahabari wakati akitangaza kuanza kwa mashindano hayo mbele ya wanahabari, Masudi Kandoro kutoka kampuni ya High Time Marketing and Promotion ambao ndio waandaaji wakuu wa shindano hilo amesema kuwa mashindano hayo yatafanyika katika Jiji la Dar es salaam tu na mashindano hayo yamegawanywa katika sehemu nne ambazo ni Kinondoni, Ilala, Temeke na Kingamboni ambapo kila sehemu kutafanyika mchujo kwa awamu mbili.

Ameongeza kuwa awamu ya kwanza itakuwa katika viwanja vya wazi kila sehemu itatoa washindani 12 kisha awamu ya pili sehemu mbili zitaungana katika mashindano ya ndani ya ukumbi ambapo kinondoni itaungana na ilala wakati temeke ikiungana na kigamboni.
Akizungumza kuhusu fainali na washindi wa shindano ilo la STAR WA SINGELI amesema kuwa fainali za mashindano hayo zitafanyika siku ya jumamosi ya tarehe 10/09/2016 katika viwanja vya Dar Live Dar es salaam kuanzia saa moja usiku ambapo siku ya fainali atapatikana mshindi mmoja kwenye washindi 12 watakaokuwa wanawania nafasi hiyo ambapo mshindi atajinyakulia zawadi ya milioni kumi.
Wanahabari wakichulkua Taarifa Hiyo 

Akizungumzia mgawanyo wa zawadi za mshindi wa kwanza amesema kuwa mshindi hatapewa Kiasi icho chote bali kitagawanywa katika maeneo kadhaa ikiwemo kupata usimamizi wa muziki chini ya HIGH TIME, Kurekodi album ya muziki wa sauti, Kufanyiwa Video tatu zenye viwango vya kimataifa, Kutangaza Muziki wa mshindi ndani na nje ya mipakaya nchi pamoja na kupewa kiasi cha Pesa Taslim.

Katika fainali hizo zitakazofanyika Dar Live zinatarajiwa kupambwa na star wa muziki huo mzee wa Hainaga Ushemeji Man Fongo na wasanii wengine wakali ambao wanaendelea na mazunguzo kushiriki.