Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO,Hassan Abbasi akifafanua mikakati yake mbalimbali kuhusiana na Idara hiyo,kwenye mkutano wake wa kwanza wa kujitambulisha na pia kuzungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo mapema leo asubuhi jijini Dar,Mkurugenzi huyo kwa mara ya kwanza leo amekutana na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali tangu kuteuliwa kwake hivi karibu.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO,Hassan Abbasi akijibu maswali mbalimbali yaliyokuwa yakiulizwa kuhusiana na mikakati yake ambayo aliitaja,kulia ni Mkurugenzi Msaidizi, Vicent Tinganya.
Baadhi ya Waandishi kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Habari,Hassan Abbasi alipokuwa akielezea mikakati yake mipya kuhusiana na Idara hiyo,mapema leo katika ukumbi wa Idara hiyo jijini Dar.PICHA NA MICHUZI JR.


                         
MKAKATI WA KUWAELEZA WANANCHI UTEKELEZAJI WA AHADI ZA SERIKALI

Dar es Salaam, Ijumaa, Agosti 19, 2016:

Serikali kupitia Idara ya Habari-MAELEZO itaanza kutekeleza mikakati mbalimbali inayolenga kuwapatia wananchi taarifa za kila mara kuhusu utekelezaji wa ahadi zake.  Mikakati hiyo itakayosaidia kuongeza uwazi na ushirikishaji, pamoja na mambo mengine, itahusisha hatua zifuatazo:-

Mosi, kuboresha mfumo wa mawaziri na watendaji waandamizi Serikalini kuzungumza na wananchi ili kuainisha utekelezaji wa vipaumbele vya bajeti, sera na mipango ya Taifa. Kuanzia Agosti 25 mwaka huu, mawaziri wataanza kuzungumza na umma kupitia vyombo vya habari kueleza vipaumbele vya bajeti zao na utekelezaji wake hadi kufikia sasa.

Pili, kuanzisha utaratibu wa Idara ya Habari-MAELEZO kueleza kwa umma kila mara, na haraka iwezekanavyo, utekelezaji wa sekta zote katika ngazi ya kitaifa. Msemaji Mkuu wa Serikali atakuwa akitoa taarifa hizo kuanzia hivi karibuni.

Tatu, Serikali itaimarisha ushirikiano zaidi na wadau mbalimbali katika kutekeleza mikakati yake ya mawasiliano kwa umma. Pamoja na wadau wengine, Serikali itahakikisha inafanyakazi kwa karibu na vyombo vya habari ili vishiriki vyema katika ujenzi wa Taifa.

Mwisho, wakati huu Idara ikiendelea kufanyiakazi mikakati mingine ili kuboresha mawasiliano kwa umma, naomba wadau wote kutoa ushirikiano kwangu binafsi, Idara niliyopewa kuiongoza hivi karibuni na zaidi tumuunge mkono Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika ajenda yake ya mageuzi kupitia HapaKaziTu.


Imetolewa na:
Hassan Abbasi,
Mkurugenzi Idara ya Habari-MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...