Mkuu wa Mwanza, John Mongella akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, wakati alipofanya ziara yake ya kwanza ya kutembelea ofisi za taasisi mbalimbali za umma jijini humo.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, namna Mfuko huo unavyofanya kazi, ambapo alisema kuwa mfuko huo sasa unawalipa mafao wanachama wake kwa wakati ambapo umevuka lengo kwa kukusanya michango ya shilingi bilioni 17.03  kati ya shilingi bilioni 17.6 za lengo kwa mwaka jana ulioishia juni 2016. Bandawe alimweleza mkuu huyo wa mkoa kuwa mfuko wa PPF umefanikiwa kusajili wanachama wapya 13,028 kwa Kanda ya Ziwa pekee ikiwa ni sawa na asilimia 105 ya lengo la kusajili wanachama 12,350 kwa kipindi cha mpaka juni 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiangalia Kadi yake ya Uanachama wa PPF aliyokabidhiwa na Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe.
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe akimkabidhi Kadi ya Uanachama wa PPF, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Ahmed Msangi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akipatiwa maelezo na Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe (shati jeupe) wakati alipotembelea moja ya Idara ya Mfuko huo, Jijini Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...