Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela jana  alitembelea eneo la Isimila na kujionea uzuri na mandhari yake. Isimila ni eneo la kihistoria lililopo mkoani Iringa nchini Tanzania, katika kijiji cha Ugwachanya kwenye kata ya Mseke kilichopo kilomita 20 kutoka Iringa mjini karibu na barabara kuu ya A 104 kuelekea Mbeya. Eneo hili ni kivutio kimojawapo kinachoupamba mkoa huu wa Iringa.
Bonde la Isimila lilikaliwa na watu tangu Zama za Mawe za Kale. Ni katika eneo hili ndipo zana za mawe za kale na nguzo za asili za Isimila zilipogunduliwa hapo tangu mwaka 1951. Pia ndani ya eneo hili mafuvu na mifupa mingi ilionekana kati yao ilipatikana mifupa ambayo ilifanana na twiga wa hivi sasa, ila tofauti ni kwamba, mifupa hiyo iliashiria kuwa twiga hao walikuwa na shingo fupi, ambapo pia kulikuwa na aina ya tofauti ya viboko.

Zana hizo zinasadikiwa kuwa zilikuwepo tangu miaka laki tatu hadi nne kabla ya Kristo. Miongoni mwa zana zilizopo katika korongo la Isimila ambalo lina mikondo miwili ni pamoja na mikuki iliyotumika kwa ajili ya kujihami na pia mawe ya kombeo kwa ajili ya uwindaji.
Pia vifaa kama nyundo zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kutengenezea zama nyingine na Shoka zilizotumika kwa kazi ya kuvunja mifupa, nyembe na visu.Kuna nguzo za kipekee zilizotengenezwa na mmomonyoko wa udongo. dalili zinaonyesha kivutio hiki kinaweza kupotea kutokana na mvua kali zikienyesha miaka ijayo.
 
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiwa katika miamba ya kale  eneo la Isimila
  Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiwa katika miamba ya kale  eneo la Isimila
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiwa katika ju,ba la makumbusho ya  kale  ya Isimila

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...