THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mheshimiwa Regina Chonjo afungua mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars

Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mheshimiwa Regina Chonjo amewataka vijana kuonyesha vipaji vyao vya soka na kutambua kuwa mchezo huo ni fursa nzuri inayoweza kuwapa maisha bora na kusaidia ukuaji wa uchumi wa nchi. 
Mheshimiwa Chonjo aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars kwa mkoa wa Morogoro uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa mchezo huo. 
“Napenda kutumia fursa hii kutoa rai kwa wazazi na walezi kuwahamasisha vijana kushiriki michuano hii ili kuendeleza vipaji vyao na kusaidia juhudi za serikali za kuinua kiwango cha mchezo wa soka hapa nchini”, alisema. Zaidi ya wachezaji  120 walihudhuria uzinduzi huo

Alisema mbali ya kuwa burudani, mpira wa miguu pia hudumisha amani, umoja, urafiki, udugu miongoni mwa viongozi na wachezaji na kuwafanya vijana kuwa wakakamavu, wachangamfu na wenye afya bora. “Lakini muhimu zaidi mpira wa miguu ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi duniani”, alisema . 
Aliwataka viongozi wa soka mkoa wa Morogoro kufuatilia kwa karibu michuano hiyo na kuchagua wachezaji wenye vipaji ili kuuwezesha mkoa huo kufanya vizuri katika fainali za Taifa za Airtel Rising Stars zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 6 hadi 11. 
Alisema michuano ya Airtel Rising Stars imekuwa ni jukwaa la kusaidia kubaini wachezaji wenye vipaji kutoka sehemu mbalimbali ambao bila mashindano haya wangeweza kupotea hivi hivi. Aliwataka viongozi wa soka mkoa humo kushirikiana na shirikisho la soka nchini (TFF) kuwalea na kuwaendeleza vijana wanaopatikana kupitia Airtel Rising Stars. 
Akiongea katika hafla hiyo ya ufunguzi, mwenyekiti wa wa chama cha Soka mkoani Morogoro Pascal Kihanga ambaye pia ni Mustahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro aliwataka vijana kucheza kwa kujituma ili kuweza kuchaguliwa kuunda timu ya mkoa. 
Kwa upande wake, Meneja wa Airtel mkoa wa Morogoro Omar Bongo alisema kuwa kampuni ya Airtel inajivunia kuweza kupata fursa ya kutoa mchango katika soka la Tanzania. “Airtel Rising Stars imekuwa chimbuko la wachezaji wa timu za Taifa na klabu hapa nchini”. Tunaona fahari kuweza kupata fursa ya kudhamini soka nchini Tanzania“alisema Bongo. 
Hafla hiyo ya ufunguzi ilishuhudia mchezo wa ufunguzi kati ya Moro Kids na Techforty ambapo Moro Kids waliibuka na ushindi wa 2-0. Katika mchezo mwingine, Mwere Kids iliishinda Kizuka 2-1.
 Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mheshimiwa Regina Chonjo akikagua timu wakati wa ufunguzi wa Airtel Rising Stars mkoa wa Morogoro kwenye uwanja wa Jamhuri. 
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mheshimiwa Regina Chonjo akipiga mpira kuashiria ufunguzi Airtel Rising Stars mkoa wa Morogoro kwenye uwanja wa Jamhuri.