Na Zuena Msuya, Arusha 
Wizara ya Nishati na Madini inafanya mnada wa Madini ya Tanzanite kwa mara ya kwanza yaliochimbwa kutoka migodi ya kampuni tano za wafanyabiasha wa madini hayo katika eneo la Mirerani Wilayani Simanjiko Mkoani Manyara. 
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa uthaminishaji na Almasi na vito Tanzania( TANSORT) Archard Kalugendo wakati wa mchakato wa kupata wafanyabiashara watakaoshinda zabuni ya kununua madini hayo kutoka Mataifa mbalimbali Duniani wakiwemo watanzania. 
Kalugendo alisema utaratibu wa kufanya mnada wa Tanzanite ni jitihada za Serikali za kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo nje nchi na pia kuwasaidia wachimbaji kuuza madini yao kwa bei halisi inayoendana na soko la dunia. 
Aidha mnada huo utaiwezesha Serikali kupata mrabaha stahiki ili kuchangia pato la taifa; vilevile kuimarisha ulinzi na usalama kwa wauzaji , wanunuzi pamoja na mali zao. Akizungumzia mnada huo, Kalugendo alisema zoezi hilo linafanyika kwa njia ya uwazi kwa kushirikisha wachimbaji, wanunuzi, Shirika la Madini la Taifa( STAMICO) pamoja Wizara ya Nishati na Madini, kwa lengo la kusimamia haki ya kila mhusika wa madini hayo. 
" Madini ya Tanzanite yanathamani ya fedha nyingi sana,kwa usalama wa wanunuzi na wauzaji, Serikali imeimarisha ulinzi wakati wa zoezi hilo ili kujihadhari na watu wasio waaminifu," alisema Kalugendo.
 Alifafanua kuwa Serikali itaendelea kuimarisha utaratibu huo ili uweze kuleta tija zaidi kwa Watanzania. Utaratibu huo ni wa kaiwaida kwa nchi zenye madini ya namna hii kama vile Zambia( emerald),Zimbabwe( Almasi) pamoja na Afrika kusini( almasi). 
Washindi wa zabuni za ununuzi wa madini ya Tanzanite wanatarajiwa kutangazwa Agosti 12 mwaka mkoani Arusha.
Mhandisi Juma Lunda( kulia) akimuelekeza mmoja wa wanunuzi wa madini ya Tanzanite kujaza fomu za kushiriki zabuni ya kununua madini hayo.
Vifaa vinavyotumika kuhifadhia Madini ya Tanzanite.
Sehemu inayotumiwa na wauzaji pamoja na wanunuzi kujiridhisha kwa kupima thamani ya madini ya Tanzanite kabla ya kufikia muafaka wa bei. 
 Mnunuzi wa madini ya Tanzanite Macmillan Njau( kulia) akijiridhisha kwa kupima thamani ya madini hayo kabla ya kununua akiwa na Mkurugenzi  wa Kampuni ya Franone Mining & Gem Company, Onesmo Mbise(katikati) ambaye ni muuzaji wa madini ya Tanzanite na Elia Benyamin( kushoto) Mnunuzi wa Madini.
Mthaminishaji Madini ya Almasi wa Serikali Edward Rweyemamu (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa mmoja wa wadau wa Madini ya Tanzanite( kushoto), Sekretari wa kituo cha Jimolojia ( TGC)Halima Hussein( wapili kulia) na Zainab Napacho (kulia)kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania( TMAA) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...