Azam Media Ltd wakishirikiana na TDE (The family of Toussaint Duches Entartainment) kutoka nchini Marekani wakiungana na vipaji vya wasanii maarufu wa sanaa ya Uigizaji Tanzania Jumapili usiku wamekonga nyoyo za mashabiki wa sanaa za maonesho jukwaani kwa onesho kali la “Souper Soul Sunday” na Igizo maalum la “Mrs Lucy Goes to Africa” kwa mtindo wa Broadway, ikishirikisha wasanii maarufu kutoka Tanzania wakiwemo “Natasha” na “Monalisa” katika ukumbi wa Jumba la Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es salaam. 
 Souper Soul Sunday ni maonyesho makubwa ya mchezo wa kuigiza ambayo imechukua sehemu kubwa ya kumbi za maonyesho na kujizolea umaarufu mkubwa Marekani. Nyota wa igizo hilo walikuwa Muigizaji/Mtunzi na Mkurugenzi mtendaji wa TDE Lady Toussaint Duchess Campbell (Lady T) akishirikiana na wasanii maarufu wa Tanzania wakiwemo “Natasha” na “Monalisa. 
 Lady T alianza kwa “kutua” Uwanja wa ndege wa Dar es salaam kamavile kwa bahati mbaya kabla ya kuchukuliwa na mwenyeji wake Natasha na kutambulishwa maisha ya Afrika, hususan Tanzania, yalivyo. 
 Igizo hilo maalum la “Mrs Lucy Goes to Africa” kwa mtindo wa Broadway, lilisindikizwa na burudani ya muziki wa Jazz na chakula maalum kilichojizolea umaarufu nchini Marekani aina ya “Gumbo”. 
 Hakika “Mrs Lucy Goes to Africa” ni igizo la kipekee na lenye kusheheni vunja mbavu na kutoa burudani kwa umati mkubwa wa wadau uliohudhuria. ''Mrs. Lucy Goes to Afrika'' ilivunjwa watu mbavu na kuwaachia ujumbe mwanana wa matumaini na faraja katika muda wote wa masaa mawili uliochezwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...