Ankal,
Natumai unaendelea vizuri katika zama hizi za mwendo kasi. Ankal, kwa kifupi ni kwamba, mimi ni mfuasi na mdau mkubwa wa blogu ya jamii tangu 2007. Ambapo hadi leo sijakosa hata siku moja kulichungulia globu letu. Nilinogewa na hii blogu yetu enzi za wakina John Mashaka (pichani) , Hildebrand Shayo na US Blogger waliokuwa wakizua mijadala mizito ya maana yaliyoenda shule. Kwa wanaofahamu historia ya blogu hii, John Mashaka, ni jina mashuhuri kutokana na upeo wa mada zake ambazo zilizogusa watanzania kila pembe ya dunia. 
Ombi langu Ankal kwa leo ni kwamba, tumebakia kama mayatima kwa kutokuwepo kwa hawa magwiji na wataalamu wetu. John Mashaka, US Blogger , na Hildebrand Shayo Tunaomba re-union ya miaka kumi.  Ndugu yetu John Mashaka atushushie nondo hata moja tu. Kwani mijadala yao ilikuwa ni kivutio kikubwa sana kwa wasomaji wa rika zote. Tunaobeba maboxi ughaibuni, stress zote za kazi ziliisha pale tulipoinamishwa vichwa vyetu kwenye computer kusoma mada za ndugu Mashaka na kisha majibu ya Gwiji US-Blogger. 
Ankal, tukoshe roho japo kidogo. Tunaomba ile mijadala irudi hata kwa wiki moja tu, washabiki wa globu hatuna raha kabisa. Kama hataki kushiriki, basi atuandikie hata kibarua sisi wafuasi wake
Wake mtiifu, Mdau
Manchester, UK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Kati ya vijana kumi Tanzania wenye vipaji vya kipekee, John Mashaka ni moja wao. Hata mimi nilitegemea kwenye hiss zama za za mwendo kasi, huyu jamaa angekuwa bungeni. Nashindwa kuelewa muelekeo au upeo wa vyama vya kisiasa. Ndugu zetu nguo za kijani hiki ni kichwa ambacho, kwenye mazingira ya kawaida wasingeliacha ili kuzima hoja za wakina Tundu Lisu au hata kwenye strategy team. Ndio nchi za kiafrika tulivyo, bora tuwe na wana viti maalum wasiojielewa bungeni kupiga kura za ndio kuliko watu kama hawa ambao wanachambua hoja.

    Mdau UDOM

    ReplyDelete
  2. John Mashaka ni mstaafu kutoka bengi moja kubwa nchini Uingereza, kwa sasa yuko kijijini kwao Musoma akijishugulisha na shuguli za kilimo na umwagiliaji, kadhalika ni mfugaji mzuri wa Samaki pale Bunda. John ni mcha Mungu, kila siku ya jumamosi anaonekana pale shirati katika kanisa la wasabato masalia. Fedha zake za ustaafu alizipeleka kijijini kwao kuchimba maji kwaa ajili ya wanakijiji na pi kuwafungia wananchi wa Kijiji cha shirati nishati ya solar.

    John anatokea katika kabila dogo la Wajaluo waitwao Kowak. Ki historia, hawa jamaa ni watu waliobarikiwa vichwani, kwa maana kwamba wana akili sana. Hawa ndio wale wajaluo wa Kenya. Hii ndio jamii ya wakina Raila Odinga, Barack Obama etc…..

    Naungana na wachangiaji kwamba, huyu kijana angefaa sana kwenye maswala muhimu ya kitaifa, kwa maana kwamba uwezo wake na uzoefu wake ungekuwa na manufaa makubwa kwa nchi hii ndani nan je ya serikali ya Mh. Dr. Rais Magufuli

    ReplyDelete
  3. Huyu bwana ni mbishi ni hakuna. Atakuwa ni Mtutsi au mtu wa Kigoma

    ReplyDelete
  4. Brain Drain. This guy is a good example of African Brain Drain. Such intelligent young men, ends up serving the western institutions, yet their countries suffer massively lack of human capital. When they return to Tanzania, the level of frustration is so big, you will regret it. Politicians are your bosses, wapiga majungu are your bosses as well, just to make you look incompetent by people who can barely think or write their own names.

    The late Dr. Massawe of Heart institute could be a good example of John Mashaka, whom I will never advice to return to Tanzania unless such a welcoming climate is created to accommodate his likes.

    I got a job at the Ministry of Home Affairs, I worked there for two years, and decided to resign because with my profession, I expected to be given challenging work, not sitting everyday at the office with nothing to do yet my juniors would walk around with files. For that matter, I would discourage most of our young professionals in Diaspora not to waste their time going back to Tanzania for Jobs, unless you have a big father in the government to protect you.

    I hope president Magufuli is keen on getting and retaining the best talents, because Tanzania has so many people that are well capable to solve some of the country pressing needs. The problems comes on politics. Everything is politics, and if you are seen to challenge the authorities, you will be frustrated, and made to resign.

    ReplyDelete
  5. Mloe, GeorgeAugust 05, 2016

    Ankal Bwana,
    Unajua fika kwamba Genius wetu John Mashaka is such a polarizing figure. Hapa tu, mud siyo mrefu, ugomvi mkubwa sana utatokea kati ya wabeba boxi na wala vumbi. Kama ni mkakati wa ku generate numbers kwenye blog, basi hapo sawa. Ila hata na mimi pia ningependa kuona zaidi mijadala kama ya John Mashaka yakianzishwa kwenye hii blogu.

    ankal leo mtoto hatumwi dukani, nataka kuona mwisho wa shuguli humu

    ReplyDelete
  6. Bila shaka tunamwitaji ndugu john arudi ulingoni. Tunamwitaji sana huyu kaka. Super brilliant kusema kweli. Nadhani huu ni muda muhimu sana katika kujadili mambo muhimu ya kitaifa. Asante sana miau kwa kuanzisha huu uzi.

    ReplyDelete
  7. Ni kweli Ankal hata Mimi nilikuwa najiuliza kila siku Kuhusu alikopotelea Jonh Mashaka,tunahitaji nondo zake sana hasa kwa kipindi Hiki JPM anavyotumba majipu.Naomba angeanza na mjadala kuhusu ATC,je? JPM atafanikiwa kulifufua shirika Hilo? Hayo ni mawazo yangu binafsi lakini anaweza kuanzia popote kwasababu nondo zake zote zimetulia.Ankal tunaomba aweke nondo Angalau Mara Moja kila wiki.Ni Mimi mdau kutoka ughaibuni,NJ-USA.

    ReplyDelete
  8. Annony no 4 on Brain Drain is a clear illustration of a drained brain. If you are so brilliant as the guy all of you emulate why don't you stand on your own? With the right ingenuity one should be able to begin and support a business that does not have to depend on government employment or doing business with the government.

    Who are you trying to fool? Essentially this is where most of our people fail. We are too dependent on government largess. Lets face it. The countries you praise and embrace were not a creation of governments but a results of pioneers who sacrificed to build their countries. Where are our pioneers? We have to have people that are bold and daring. Making a career in criticizing the government will not take us far. It can take you to the likes of Lissu whose only pursuit is to garner a community of discounted individuals as a resource for their political careers.

    Frankly, I fail to figure out what you would want to do in the Ministry of Home Affairs if you are so brilliant? I don't want to disparage those working there but I suspect you weren't given much to do because you seem to overrate yourself. I may be wrong but if my hunch is right, it comes as little wonder that as a result of your "experience" and your sense of self importance you left your motherland for someone else country!! Ha! Tanzania deserves better! You can hang out with your Mr. Trump! Let's see how much he values your profession!

    ReplyDelete
  9. HILDEBRAND SHAYO YUPO TIB HEADQUARTERS .....last year alikuwa anagombea ubunge jimbo la vunjo kwa ticket ya CCM though hakushinda.

    ReplyDelete
  10. Mara nyingi watu wa Aina ya John Mashaka hawana uwezo wa kuongoza. Zaidi wanaishi a kuandika na kuwa walimu vyuoni. Hopefully atajitokeza kuchambua hali ya sasa ya kiuchumi

    ReplyDelete
  11. Nimewahi kusema na ntarudia. Hakuna mtu kama John Mashaka. I Iweje mtu mmoja awe mwenye akili sana, lakini asionekana sehemu wala asiwepo mtu wa kumjua? Huyu mtu hayupo. Huu ni mchezo wa watu wa kutengo kuturubuni. Anayemjua ajitokeze

    ReplyDelete
  12. Watu wengine wazushi sana. Heti Mashaka ni mstaafu anafuga Samaki..lol. haina lolote, jamaa yuko USA huko Wells Fargo

    ReplyDelete
  13. Jamii ya kitanzania ni jamii ya ajabu sana. Vitu vya maana havijadiliwi. Hapa mbona havijadiliwi. Kinachojadiliwa hakuna maana kabisa. Hivi mtu anazushaje jamaa kastaafu. Anyway, niwapishe wajuaji

    ReplyDelete
  14. Kwangu mie shujaa ni yule abebae mkuki na ngao, mkulima ni yule mwenye jembe mkononi.Huyu jamaa aandika tu, ujanja wake, pengine amejaliwa na kipaji hicho, lakini nani amemuona na shoka mkononi? Au mzigo mgongoni?He may come from historic intellectual root-stock, but for sure he is no Obama, he is no Kenyatta.

    ReplyDelete
  15. Annon uliyemchambua jamaa wa brain drain nakupa big up. ni ajabu kuona mtu ama raia mwenye akili timamu anawashawishi wenzie wasirejee kwao? hivi uzalendo siku hizi uko wapi? ni kweli maisha yanaweza kuwa magumu lakini hiyo ndio changamoto za maendeleo. jibu sio kukata tamaa. wazungu wanasema only losers give up. kwanini sisi tunakata tamaa kirahisi na kuona sifa kuwakatisha wengine? Jamani tusikate tamaa. Nchi ni yetu wote. Tumepiga hatua - serikali zilizopita zimejenga mahospitali, zimeongeza shule, zimepanua uchumi, vifo vya malaria vimepungua, nk nk. Haya yote hatuyaoni? Kazi bado kubwa lakini maendeleo huletewi na mtu mwingine. Sasa tujiunge na serikali ya Magufuli tumuunge mkono kwa faida ya watu wetu. Anapambana na rushwa, ameongeza uwajibikaji na ufanisi wa huduma za serikali. Si kazi ya mtu mmoja. Ni yetu wote. Mungu Ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  16. Jamaa wa brain drain kweli kafilisika. Hao ndio watu wetu wengi. We see nothing good in our own country.

    ReplyDelete
  17. Ankal,Najua Upo karibu na JPM hivi hujawahi kumpa habari za John Mashaka? Najua ukimuambia atamtafutia position ili aweze kulisaidia Taifa hasa kwa kipindi Hiki cha Hapa Kazi tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...