MSANII wa muziki kutoka nchini Nigeria Omo Alhaji,Jagabana maarufu YCEE,ametoa msaada wa shilling million 1,kwa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha Kigamboni Community Center(KCC).

Akizungumza katika ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo leo jijini Dar es salaam mratibu wa ujio wa msanii huyo bi Salha Kibwana amesema kuwa msanii YCEE ametoa msaaada huo katika kituo hicho kwa lengo la kusaidia watoto hao ili kujipatia mahitaji maalum ya kila siku wawapo kituoni hapo.

“Ametoa msaada huo kutokana na faaida anayopata katika kazi zake usanii ili kukuza vipaji na kujenga upatikanaji wa elimu wa elimu kwa jamii hasa ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi,”alisema Salha

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Mkurugenzi wa kituo hicho Mbwana Msangule,amesema kuwa kituo chake kinalea watoto hao ili kuwasaidia kuondokana na maisha magumu yanayowakabili.

“msaada huu utasaidia sana kwasababu kituo kina watoto 14 wanaoishi kituoni hapo na wengine wanakuja na kurudi makwao,na nashukuru sana kwa msaada huu kwani ni sanii wa kwanza kutoka msaada,nawaomba pia wasanii wa ndani kijitokeza kutoa msaada”alisema Mbwana

Kwa upande msanii huyo amesema kuwa amekuja kutembelea Tanzania ili kujifunza na kuonana na wasanii wengine wakubwa wa Tanzania huku akiwataja Diamond na Ali Kiba,ameongeza kuwa amefurahi pia kuktana na mashabiki wake ambao amekua wakichati kupitia mitanzandao ya kijamii.
 
Msanii Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE kutoka Nigeria akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha Kigamboni Community Center Mbwana Msangule(kushoto) leo Jijini Dar es Salaam Katikati ni Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt.Msanii hyo yupo nchini kufuatia ziara yake kwa Vyombo vya Habari inayoratibiwa na Kampuni ya Mahusiano ya Umma ya LAS Consultancy.

Mwanzilishi wa Kampuni ya Mahusiano ya Umma, LAS Consultancy Bi. Salha Kibwana akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ziara ya msanii Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE (hayupo pichani) leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt na Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha Kigamboni Community Center Mbwana Msangule. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tinny Entertainment kutoka Nigeria Arokodare Timilehin akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani kuhusu ziara ya msanii Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE (wa tatu kutoka kushoto) leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha Kigamboni Community Center Mbwana Msangule na Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt. 
Msanii Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE kutoka Nigeria akizungumza na  waandishi wa habari kuhusu ziara yake katika Vyombo vya Habari inayoratibiwa na Kampuni ya Uhusiano wa Umma ya LAS Consultancy ya Jijini Dar es Salaam leo.Kutoka kushoto ni Mwanzilishi wa Kampuni ya LAS Consultancy Bi. Salha Kibwana, Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto cha Kigamboni Community Center Mbwana Msangule na Meneja Miradi wa Tinny Entertainment Oladaro Pratt. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina ya uongozi wa LAS Consultancy walipokuwa wakimtambulisha msanii kutoka Nigeria Omo Alhaji, Jagabana maarufu YCEE ambaye yupo nchini kwa ajili ya ziara ya kutembelea Vyombo vya Habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...