THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Msimu wa pili wa Kambi tiba ya GSM waanza kazi Mtwara

Timu ya Madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Mi9fupa na upasuaji kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tayari iko mkoani Mtwara na leo hii wameanza kazi ya kuwafanyia upasuaji wa bure kabisa watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi chini ya udhamini wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya GSM Foundation.

Kwa mujibu wa Mratibu wa zoezi hilo linalotarajiwa kufanyika nchi nzima, Dk Othman Kiloloma ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa MOI, zoezi hilo kwa mkoa wa Mtwara peke yake litachukua siku nne ambapo litakuwa likifanyika katika Hospitali ya Ligula, ambapo pamoja na mambo mengine, madaktari wanaofanya kazi katika hospitali hiyo watapewa mafunzo ya jinsi ya kufanya upasuaji wa namna hiyo ili kupunguza tatizo la vifo kwa watoto hao ambao madaktari wa kuweza kuwatiobu wako tisa tu nchi nzima na kati yao nane wapo Dar es Salaam na mmoja tu yuko Bugando, Mwanza.

Kwa upande wake Afisa mawasiliano wa Taasisi ya GSM, Khalfan Kiwamba amelieleza lengo la Taasisi yake kuwa ni kuokoa angalau asilimia 10 tu ya watoto wanaosadikika kupoteza maisha kila mwaka kutokana na changamoto ya kuzaliwa na kichwa kikubwa ama mgpongo wazi, ambapo wengi wao hukosa tiba kutokana na imani za kishirikina, na wakati mwingine sababu za kiuchumi.

Inasemekana takriban watoto 4000 huzaliwa kila mwaka nchini wakiwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi, lakini wanaorudi mahospitalini kwa ajili ya matibabu huwa hawazidi 500, hali inayosababisha wadau wa afya kuamini kwamba aidha watoto waliobaki hupoteza maisha, ama kupata mtinfdio wa ubongo.
 Mkuu wa msafara wa madaktari Dk Kiloloma(kushoto), kutoka MOI, akitoa maelezo kwa Katibu Tawala wa mkoa wa Mtwara, kulia ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Mtwara Dk Sichalwe
 Uongozi wa kambi ya Upasuaji kutoka GSM Foundation na MOI ukijieleza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi Halima Dendegu
Picha ya pamoja kati ya timu ya Kambi tiba ya Upasuaji, Katibu Tawala na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara