Kambi tiba ya GSM iliyokuwa imeingia katika msimu wake wa pili tangu Agosti mosi mwaka huu, imefungwa rasmi mkoani Iringa, huku watoto 37 wakiwa wamefanyiwa upasuaji, na wengine zaidi ya 300 wakipata ushauri nasaha kutokana na afya zao kutoruhusu kufanyiwa upasuaji, huku suala la uimara wa afya likiwa kipaumbele cha kwanza.

Awali akiongea kabla hajamkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Bi Amina Masenza kuongea, Msemaji wa Taasisi ya GSM, Khalfan Kiwamba alisema kila kukicha wanashukuru kuona maisha ya watoto ambao ilikuwa wapate mtindio wa ubongo ama kupoteza maisha yanaokolewa kupitia mchango wao pamoja na madaktari kutoka Taasisi ya ya Mifupa na upasuaji ya Muhimbili, MOI.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI kwa mwaka 2002, unasema zaidi ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na vichwa vikubwa na migongo wazi, na kati yao ni 500 tu wanaoweza kufika hospitali na kupata matibabu kutokana na changamoto kuu tatu.

Ya kwanza ni uhaba wa madaktari bingwa wa upasuaji wa vichwa vikubwa na vikubwa na migongo wazi ambapo kwa tanzania nzima, kwa sasa wamebaki saba tu, huku sita wakiwa ni waajiriwa wa Taasisi ya MOI na mmoja akiwa hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza.

Kutokana na uhaba huo wa madaktari, ambao wanapatikana katika mikoa miwili tu ya Tanzania, Mikoa mingine ambayo watoto wa aina hii huzaliwa wagonjwa hupata changamoto ya pili ya kusafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu ambapo hata hivyo, wakifika huko hupata changamoto ya kukuta foleni ya wagonjwa kutoka mikoa mingine wanaokuwepo kutoka mikoa mingine.

Kuna imani pia za kishirikina ambapo watoto wengi hupelekwa kwa waganga, wakihisi labda wamelogwa, wakati hili ni tatizo la kiafya ambalo mtoto akiwahishwa anaweza akawahishwa hospitali na akapona,

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Iringa, Bi Amina Masenza amewaomba GSM Foundation warudi tena iringa kwani anahisi wagonjwa waliotibiwa kutoka mkoa wake ni wachache sana, ukilinganisha na idadi anayoijua ya watoto waliomo mkoani humo.

Mkuu huyo ametoa maagizo kwa wakuu wa wilaya kuhakikisha kwamba wanajua idadi ya wagonjwa waliomo katika wilaya zao ili waeze kuwatayarisha kwa ajili ya matibabu kabla hajawasiliana na wataalamu ili kulimaliza tatizo hilo kama sio kulimaliza kabisa.

PICHANI JUU: Msemaji wa GSM Foundation, Khalfan Kiwamba `Kiwadinho',(Kulia) akiongea na wanahabari(Hawapo pichani), huku akishuhudiwa na Meneja wa Meneja wa Taasisi hiyo Shannon Kiwamba(Wa kwanza kushoto), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Robert Salim(wa Pili kutoka kushoto, na Kibwana Matukio kutoka GSM Foundation(Mwenye Miwani).
 Mkuu wa Mkoa wa iringa, akimjulia hali mmoja kati ya watoto waliofanyiwa upasuaji na mmoja kati ya watoto waliofanyiwa upasuaji na Kambi tiba ya GSM Foundation.
Dk Mwanaabas Sued kutoka Taasisi ya MOI, akiongea na wanahabari(Hawapo pichani), huku akishuhudiwa na Afisa Miradi kutoka GSM Foundation Kibwana Matukio(wa Kwanza kushoto) Dk John Mtei kutoka MOI,(wa Pili kutoka kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela (kushoto).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...