MTU mmoja amefariki dunia jana  baada ya kugongwa na geti la lango la kuingilia treni Stesheni jijini Dar es Salaam, Ajali hiyo imetokea baada ya   Marehemu kunining’inia nje ya behewa wakati wa treni ya Pugu ilivyokuwa  ikitoka eneo la  stesheni majira ya jioni.

Katika Taarifa ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) iliyotolewa na na Afisa ya Uhusiano Kwa niaba ya  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Focus Makoye Sahani  imeeleza kuwa  tofauti ya usafiri wa basi ni kuwa na kondakta anaweza kusimamisha basi ili kumshusha mtu anayening’inia nje lakini kwa treni jinsi ilivyo ndefu  hilo haliwezekani.

Pia ametoa wito kwa wasafiri  na wananchi kwa jumla wanaotumia usafiri huo  kufuata masharti ya usafiri ili kuepuka maafa yaliyomkuta mwenzetu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kikosi kazi cha TRL hapo kesho Agosti 5, 2016 kitaanza kampeni za kuwahamasisha wananchi wanaofanya shughuli  katika maeneo  ndani ya mita 15 za tuta la reli kuhama kwa hiyari. 

Hatua hiyo inachukuliwa ili kuwaepusha wananchi hao na uwezekano wa kupata madhara endapo ajali ya treni kuacha njia itatokea na pia kulinda tuta la reli dhidi ya mmonyoko unaosababishwa na shughuli za kibinadamu za kila siku . Kikosi kazi hicho kitahusishwa Idara ya Usalama na Ulizni wa reli na Kikosi cha Polisi TRL.

Watumiaji wa huduma za usafri wa treni za abiria za Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) wametakiwa  kuzingatia  sheria za matumizi ya usafiri huo ili kuepuka adhabu ya kufungwa jela miezi sita.

Nae   Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Polisi TRL ACP Mary Lugola amesema matumizi ya usafri wa abiria unasimamiwa na sheria , kanuni ,taratibu na masharti maalum. Mojawapo amelitaja ni kutodandia mabehewa baada ya milango kufungwa.

‘Endapo mtu atafanya kosa hilo atafikishwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita”.Alisisitiza Afande Lugola.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kwa nini hatutaki kujifunza ustaarabu wa kupiga foleni mahali kama hapa.
    Ugombaniaji kama huu ni hatari kwa abiria, pia mara nyingi unawapa fursa pick-pockets kufanya ufundi wao

    ReplyDelete
  2. Nikuzuia asiwepo anayening'inia tukawie tufike hakuna haja ya kuhatarisha maisha kwa kuning'inia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...