Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Dar es salaam
Tofauti
za kisiasa zilizopo nchini zisivuruge nuru ya amani iliyojengwa tangu
enzi za Serikali ya Awamu ya Kwanza ambapo siasa za nchi zililenga
katika umoja, amani na ujenzi wa Taifa imara, anaonyesha mmoja wa walimu
wa diplomasia nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia nchini (CFR), Dkt.
Bernard Achiula wakati wa mahojiano na Mwandishi wa habari hii kuhusu
hali ya siasa nchini kwa sasa na ushiriki wa watanzania kwa ujumla
katika kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano katika utatuzi wa
changamoto za kimaendeleo badala ya kuanzisha tabia za vurugu na
maandamano.
Dkt.
Achiula amesema kuwa uwepo wa amani nchini unachangia katika kuvutia
wawekezaji nchini, kukuza utalii wa ndani, kuvutia wahisani kutoa
misaada kwa kuchangia katika uanzishaji na uendelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo hivyo kila raia nchini bila kujali itikadi yake
ya dini wala chama ana budi kuilinda amani iliyopo.
“Tofauti za kisiasa zipo katika kila nchi kulingana na mitazamo tofauti iliyopo ila kinachotakiwa ni kuweka taifa mbele kwa manufaa ya nchi, watanzania tunatakiwa kuwa wazalendo ili kuimarisha umoja na amani iliyopo kwani vitu hivi vinategemeana na hatimaye kuiwezesha Serikali ya awamu ya tano kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea maendeleo.
“Tofauti za kisiasa zipo katika kila nchi kulingana na mitazamo tofauti iliyopo ila kinachotakiwa ni kuweka taifa mbele kwa manufaa ya nchi, watanzania tunatakiwa kuwa wazalendo ili kuimarisha umoja na amani iliyopo kwani vitu hivi vinategemeana na hatimaye kuiwezesha Serikali ya awamu ya tano kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea maendeleo.
“Tofauti
hizo zisiwe chachu ya kuvuruga amani tuliyonayo bali watanzania kwa
ujumla tunatakiwa kuitunza amani hii iliyojengwa tangu enzi za Mwalimu
Julius Nyerere ili kuweza kuvutia wawekezaji na utalii katika nchi
yetu” alifafanua Dkt Achiula.
Alisema
kuwa haoni sababu kwa vyama vya siasa nchini kuandaa maandamano
yanayolenga kuvuruga amani iliyopo kwani kikubwa kinachotakiwa kwa
wananchi ni misingi mikuu ya maendeleo ikiwemo elimu, afya na huduma
bora mbalimbali ambapo Rais Magufuli ameanza kuvifanyiakazi.
Akizungumza
kuhusu Balozi zetu nje ya nchi Dkt Achiula aliwashauri mabalozi hao
kuzidi kuitanganza nchi yetu ya Tanzania ili kuweza kuvutia wawekezaji,
utalii na biashara ili kusaidia katika ukuuaji wa sekta ya viwanda
ambapo Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuipeleka nchi katika uchumi
wa viwanda.
Akizungumzia
utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano Dkt Achiula amesema kuwa Rais
Dkt. Magufuli amejikita katika kutatua changamoto zinazolikabili taifa
kwa muda mrefu ikiwemo kupiga vita rushwa, kuongeza ukusanyaji mapato
kwa kuwabana wakwepa kodi, kubana matumizi ikiwa nia ni kuimarisha
uchumi wa nchi na kuipeleka nchi kwenye uchumi wa Kati.
ReplyDeleteNaunga mkono kwamba hakuna sababu ya maandamano hasa pale yanapokuwa yamepigwa marufuku na utawala. Jambo la msingi ni kusulisha migororo kwa mazungumzo na vyombo kama mabaraza mbali mbali likiwepo Bunge.
Nadhani ni haki "KUBWA" sana ya Kikatiba kwa Wawakilishi wetu kutumia chombo hiki kutatua matatizo ya Taifa hili kuliko haki ya Kikatiba ya kuandamana.
Binafsi nampongeza Dkt Achiula hasa pale aliposema haijalishi ni jumuiya ngapi sisi kama nchi tumejiunga bali swali la kujiuliza ni Tunajua tunachokitaka katika hizo jumuiya?
Nawasilisha.
kusingetolewa amri ya kuzuia mikutano na maandamano bila shaka tusingefika hapa. Mwalimu Nyerere alipata kutuasa tuwe na utaratibu wa kujisahihisha. Kinachotakiwa kuruhusu mara moja na bila masharti yoyote mikutano na maandamano na nina hakika hilo likifanyika huu mzozo na tishio la amani yetu halitakuwepo.
ReplyDelete