Mwanamitindo mstaafu wa kimataifa Tausi Likokola, ambaye yupo hapa nchini, ana miradi mbalimbali  inayoendelea, kwa sasa anazindua kipindi chake cha Television, chenye malengo ya kuwainua wasichana na wanamitindo kwa jumla kwa kutumia ulimbwende, fasheni na uanamitindo kama mwamvuli.  

Tausi ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kukuza vipawa vya wasichana ulimwenguni kote kwa kutumia uzoefu wake katika fasheni, mitindo uandishi wa vitabu na ujasiriamali, anasema ni wakati sasa wa kufanya hayo hapa nyumbani kwao mwenyewe.
Kipindi kinaitwa ‘TAUSI LIKOKOLA’S AFRICAN PRINCESS MODEL SEARCH’ ambacho kimetokana na wazo lililobebwa katika vitabu vyake viwili, T’he African Princess’ na kingine cha ‘Beautiful You’. 
Kipindi hicho cha kwanza na cha aina yake, kitaanza kurushwa katika kituo cha televisheni cha TV1 kuanzia IJumaa ya Agosti 5, 2016 saa 10:00 jioni na kurejewa tena Jumapili asubuhi.
Tausi anaamini kwamba wasichana wanahitaji kufundishwa na kutiwa moyo kuelekea katika ndoto zao, na kipindi hiki kitaonesha vipengele tofauti tofauti katika maisha kuanzia maadili, ulimbwende, nidhamu na mambo mengine, hiki ni kipindi kwa familia nzima.
Lengo kuu la Tausi Likokola’s African Princess Model Search ni kukuza na kuongeza uwezo wa msichana mmoja mmoja katika stadi za uongozi na uwezo katika kujitambua, kujikubali, kujiamini na kuwa na mawazo chanya na kujifunza stadi za mawasiliano mazuri ambayo hatimaye yatafanya washindani kufanikiwa sana katika maisha yao ya baadaye katika ulimwengu wa ushindani wa fasheni.
Tausi aliyezindua bidhaa kadhaa za urembo na maisha kupitia kampuni yake ilipo Tanzania,ijulikanayo kama ‘Tausi Dreams Ltd. Tausi anayeishi Marekani bado, yupo hapa nchini kwa sasa kuendeleza miradi mbalimbali ikiwepo bidhaa zake zilizoanshishwa hivi karibuni ikiwemo pafyumu yake inayoitwa Tausi Dreams ikiwemo nywele za binadamu zinazoitwa Tausi Beautiful You Hair.

Tausi aliyekulia katika ulimwengu wa fasheni kimataifa katika miaka ya 90, amefanya kazi na makampuni makubwa ya mitindo kama Gucci, Christian Dior, Issey Miyake, Tommy Hillfger, Escada na wengine wengi, na sura na kazi zake kupamba kurasa za mbele na za ndani katika magazeti na majarida kadhaa ya mitindo na maisha ya kimataifa na hapa nyumbani, amekuwa akiwatia moyo wanamitindo wengi hapa nchini na wengine duniani kote. 

Tausi amefanikiwa sana kulitumia jina na kipawa chake kuwasaidia watu wake wa Tanzania katika elimu, kutambua UKIMWI, mahitaji ya jamii, na ameweza kuchangia katika kukua kwa utalii katika nchi yake ya kuzaliwa (Tanzania), kibiashara na kukuza maliasili. Tausi ana mpango wa kusimamia kazi kadhaa za kujitolea kupitia kampuni yake ya ‘Tausi and Friends for Life’
Tausi alipumzika kujitokeza katika uanamitindo ili kupata muda mzuri wa kukaa na familia. Wakati wa kazi za mitindo Tausi ametembelea nchini nyingi za Afrika, Ulaya, Asia, Australia na kwa sasa akiwa anaishi Marekani. Tausi ameandika vitabu vinne hadi sasa akitumia uzoefu wake uliopata toka mataifa mbalimbali akifanya kazi na wasichana toka ulimwenguni kote kuwasaidia kwa hali na mali. Vitabu alivyotoa hadi sasa ni; The Art of the Beauty and Health’,  The African Princess,’ ‘The Touch of an Angel’ na ‘Beautiful You’.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...