Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama Kiss Daniel akionesha albamu yake kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mkutano wa kutambulisha uwepo wake katika Tamasha linalozinduliwa jijini Dar es salaam siku ya kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee, Posta jijini Dar es salaam.
  (Kutoka kulia) Mkurugenzi wa Stra8up Vibes, Sniper Mantana ambao ni waandaaji wa Tamasha la “Monte Carlo Classic’ akizungumza na waandishi wa habari (hawapo) pichani wakati wa kumtambulisha Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama ‘Kiss Daniel’atakayepamba uzinduzi wa Tamasha hilo litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam. Pamoja nae ni Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera, Msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel, mbia wa Tamasha hilo kutoka Malaysia DeJurist Global na Meneja wa Msanii huyo Louiza Williams.
 Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera akizunguzmza katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kumtambulisha Msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel atakayepamba uzinduzi wa Tamasha la “Monte Carlo Classic” litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam. Benki ya Barclays ni wadhamini rasmi wa Tamasha hilo ambalo limezinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
 Mmoja wa washiriki katika uandaaji wa Tamasha la Monte Carlo Classic DeJurist Global kutoka Malaysia akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya kumtambulisha msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel ambaye yupo nchini kwa ajili ya kupamba uzinduzi wa Tamasha hilo litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Akemi ulipo katika jengo la Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam. Pamoja na kulia ni Msanii kutoka Nigeria Kiss Daniel, Meneja masoko wa benki ya Barclays, Joe Bendera na Mkurugenzi wa Sta8up Vibes, waandaji wa Tamasha Sniper Montana. Benki ya Barclays ni wadhamini rasmi wa Tamasha hilo ambalo limezinduliwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
 Msanii maarufu kutoka Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel almaarufu kama Kiss Daniel akifurahia jambo na Meneja Masoko wa benki ya Barclays Joe Bendera (kushoto) sambamba na Mkurugenzi wa Stra8up Vibes Sniper Mantana (katikati) mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari wa kumtambulisha msanii huyo atakayepamba uzinduzi wa Tamasha jipya nchini la “Monte Carlo Classic” litakalofanyika kesho kwenye ukumbi wa Akemi uliopo Golden Jubilee Towers, Posta jijini Dar es salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
Mwanamuziki maarufu wa Nigeria Anidugbe Oluwatobiloba Daniel anayefahamika kwa jina la kisanii Kiss Daniel aliyetamba hasa kwa kibao cha ‘Woju’ kwenye anga za muziki,  ametua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa Monte Carlo Classic tukio lililoandaliwa na Str8up Vibes wakishirikiana na DeJurist Global kwa udhamini wa Benki ya Barclays Tanzania.

Mwimbaji huyo wa Nigeria aliyejizolea mashabiki wengi tangu alipoachia kibao chake cha ‘Woju’, ataongoza uzinduzi wa tukio hilo Jumamosi hii jijini Dar es Salaam katika Mgahawa wa Akemi uliopo kwenye jengo la Jubilee Towers, Mtaa wa Ohio.

Akizungumza mapema hii leo kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Str8up Vibes, Sniper Mantana alithibitisha mbele ya waandishi kwamba maandalizi ya tukio hilo yamekamilika na kuwasihi Watanzania kujitokeza kwa wingi ili kujumuika na msanii huyo maarufu.
Aliongeza kwamba kabla ya tukio hilo tiketi zitauzwa kwa shilingi 25,000 na itakapo timu usiku tiketi zitauzwa kwa shilingi 35,000.

Alisema tukio la the Monte Carlo Classic limelenga kubadilishana uzoefu baina ya Watanzania hususani kwenye sekta ya burdani.

“Kwenye miji kama vile;-Monte Carlo, New York, Los Angeles (L.A), Paris watu maarufu hushiriki kwa kupamba matukio kama haya. Hii ni sawa na ambavyo sisi tumelenga kuliimarisha tamasha la Monte-Carlo Classic jijini Dar es Salaam, ambapo kwa usiku mmoja kila mtu anakuwa mtu wa hadhi ya juu, huku akisherehekea na mtu maarufu aliyeteuliwa na kwenye eneo lenye hadhi ambalo limeandaliwa na waandaaji,” alisema.

Nae Meneja Masoko wa Benki ya Bacrays Tanzania, Joe Bendera, alisema benki hiyo imekuwa ikidhamini ligi kubwa ya soka ulimwenguni jambo ambalo limeifanya kuisogeza karibu na jamii benki hiyo. Tunayofuraha kuwa sehemu ya uzinduzi wa tukio hili kubwa jambo ambalo litatuwezesha kukutana na wageni waalikwa mbalimbali na wateja wetu.

"Tukio hili linatupa fursa ya kutoa elimu kuhusu matumizi ya kadi zetu na kuhamasisha matumizi yake sehemu mbalimbali kwenye mashine za mauzo maeneo mbalimbali nchini. 

Mwezi uliopita Benki ya Bacrays ilitunukiwa cheti cha ubora cha Mtoaji wa Kadi Bora za Visa nchini Tanzania. Kubeba fedha taslimu kuna kiwango maalumu hivyo tunapenda kuwahamasisha kadi zetu za Debit na Cretid kwenye tukio hili," alisema
Kwa upande wake msanii huyo alisema alishtuka alipopata mwaliko kutoka kwa Str8up Vibes na kumchague yeye kuwa mgeni rasmi kwenye tukio hilo, na kwa mara ya kwanza kuja hapa nchini kama msanii.

 “Nimefuarahi sana kualikwa kwenye tukio la Monte Carlo Classic hapa jijini Dar es Salaam, ninashukuru kwa nafasi hii na ninapenda kuwashukuru waandaji kwa kutambua umuhimu wangu.”

Msanii huyo aliongeza kwamba, amekuja nchini kufurahia na kujumuika na watu hadhi tofauti, wasanii wa muziki pamoja na mashabiki zake na kuwaomba wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kufika kwa wingi siku ya Jumamosi kwenye tukio hili.

Kwa hivi sasa amejiunga na lebo ya G-Worldwide Entertainment iliyomwezesha kurekodi nyimbo zake tatu; Woju, Mama na aliouachia hivi karibuni wa Jombo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...