“Napenda kuvishauri vyama vya siasa nchini kuacha kutumia kauli za kibabe na vitisho kwa kisingizio cha kutumia haki zao za kikatiba, hali hiyo itapelekea vyombo vya dola kuchukua hatua kwani ni viashiria vya uvunjifu wa amani”. Amesema Mh.Masaju.
 Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),George Masaju alipokuwa akizungumza nao masuala mbalimbali yaliyohusu wajibu wa Utii wa Sheria na kudumisha amani nchini,alipokuwa akizungumza mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar leo.

 Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG),George Masaju akifafanua masuala mbalimbali kuhusu wajibu wa Utii wa Sheria na kudumisha amani nchini,alipokuwa akizungumza mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar leo.PICHA NA MICHUZI JR

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar leo,Masaju amesema kuwa polisi wamesema kuwa wana hali ya kuzuia mikutano na maandamano iwapo watabaini kuwa yataibuka mambo yatakayohatarisha amani ya nchi,Masaju amesema kuwa maandamano hayo yataleta madhara na athari kama maandamano hayo ya UKUTA-Septemba mosi mwaka huu.

Amesema kuwa madhara na athari ya maandamano hayo ni kubwa kutokana na siku hiyo itakuwa mahsusi kwa ajili ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwao,akaonngeza kuwa siku hiyo kutakuwa na tukio muhimu la kupatwa kwa Jua huko Lujewa mkoani Mbeya ambapo ni muhimu kwa nchi kupata manufaa kwa Watalii kuja kwa wingi na kuweza kunufaika Kiuchumi. 

Masaju amesema kuwa vyama vya siasa nchini vinatakiwa kutumia vyema haki zao za msingi zilizoanishwa katika katiba badala ya kutumia, nguvu, ubabe na kupelekea kutishia hali ya amani na utulivu iliyopo nchini.

Masaju amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya wanasiasa wanaotoa vitisho vya kuitisha mikutano kinyume na taratibu za kisheria kwa kisingizio cha haki za kikatiba jambo ambalo sio kweli.“Napenda kuvishauri vyama vya siasa nchini kuacha kutumia kauli za kibabe na vitisho kwa kisingizio cha kutumia haki zao za kikatiba, hali hiyo itapelekea vyombo vya dola kuchukua hatua kwani ni viashiria vya uvunjifu wa amani”.

Masaju aliwataka Wanasiasa kuwa wakweli na kuacha kuwapotosha wananchi kuwa wananyimwa haki ya kufanya mikutano kwani wapo baadhi yao wanaofanya mikutano katika majimbo yao baada ya Jeshi la Polisi kujidhirisha kwamba kutakuwa na hali ya amani na utulivu”. Alisema Mhe. Masaju.

Aidha Masaju alipongeza juhudi zinazofanywa na viongozi mbalimbali wa dini nchini kwa jitihada wanazofanya za kushauri katika kufika muafaka wa hali ya kisiasa nchini na kuwashauri kuhubiri amani na utulivu kwa waumini wao. 

Akitoa ufafanuzi wa tamko la baadhi ya vyama vya upinzani kutaka serikali kuvifuta vyama hivyo Mhe. Masaju alisema kuwa suala hilo ni kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu katiba hiyo inaruhusu mfumo wa vyama vingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Amani iliyopo inatosha kwa haki zote kupatikana wala hakuna atakayeivunje hata akiandamana mwaka mzima.

    ReplyDelete
  2. Mbona mikutano ya siasa imekuwepo tangu 1992 lakini amani haikuvunjika wala watu hawakuacha kazi?

    ReplyDelete
  3. Inasikitisha kupoteza askari kwa mauwaji.

    Lakini polisi wengi hudhulumu wananchi, hata raisi alitoa hotuba kuwa kuna kesi za kubambikizwa, raia wamechoka, ndo maana jambazi wauwaji waovu wanaonekana kwa wananchi kadhaa kama wanawasadia kisasi. japo nakubali muono huo ni mbaya na mwovu. Lakini polisi wafate ushauri wa raisi.

    ReplyDelete
  4. Rais alizuia mikutano ya kisiasa kwanza kabla ya ukuta na kabla ya zuio la polisi kuzuia ukuta.

    Rais hakuzuia mikutano kwa kukemea ukuta. Ni miongoni mwa mbinu zake za kutekeleza "kauli mbiu" yake ya hapa kazi tu. Ili watu wafanye kazi tu.

    Naona Mh mwanasheria umeteleza kidogo hapo uliposema katazo la polisi ni baada ya kupewa habari na polisi kuhusu uvunjifu wa amani. Raia wakiona uongo unafanya waone chadema nafuu. Uko upande wa sheria basi sema kweli, usidhani ukisema ukweli utatumbuliwa. Ukimtetea raisi kwa uongo anaweza kukutumbua yule, hapendi uongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...