THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MWENYEKITI MAGUFULI INGIA UVCCM KUNA MAJIPU YAMEIVA,UNDA TUME - MWAKIBINGA

video

Wasalaam, 
Ndugu zangu Waandishi wa Habari wa Hapa Makao Makuu ya Tanzania Yetu Dodoma.
  Lengo la Kuwaita Hapa Leo kwanza Kumpongeza Mwenyekiti Wetu wa CCM ambaye ni Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kuchaguliwa kwa Kura nyingi na Wajumbe wa Mkutano mkuu Kukiongoza Chama chetu  cha Mapinduzi, Pili Kuongoza Taifa letu Tanzania kwa kurudisha nidhamu kwa Watumishi wa Umma na Mali za Umma kutoshezewa ovyo, Ukusanyaji wa Mapato ya ndani, Elimu bure ambayo imeambatana na Kampeni iliyofanikiwa asilimia 97 ya Madawati, Kujali wanyonge katika kuendelea kuboresha huduma bora za Kijamii, Kushughulikia Kikamilifu suala la Rushwa na Ufisadi kwa kuunda Mahakama Maalumu ya Kushughulikia kesi za Mafisadi na Wahujumu Uchumi..

  Ndugu Waandishi wa Habari, Leo Ijumaa  wakati  wa Mapokezi ya Mwenyekiti Wetu Mh.Rais Dkt.Magufuli ameendelea kuonesha uchungu wake Juu ya Chama chetu kuhusu Mapato ya Jumuiya za ndani ya Chama ikiwa  mambo kadhaa ambayo baadhi ya Viongozi wamekua ni Miungu watu, wamekua wakitumia Mali za Chama na Jumuiya zake kwa maslahi yao Binafsi.

  Ndugu Wanahabari naomba sasa WANACCM nchi nzima tumsaidie Mwenyekiti Wetu kuwabainisha watu wenye dhamira ovu na Matendo yasiyofaa ndani ya Chama chetu ambao wanakiuka katiba,  taratibu na kanuni za Chama chetu cha Mapinduzi kuhusu Mali za Chama, Miradi ya Chama ambayo wamekua Wakiifanya kama sehemu yao ya Kujiingizia Kipato.
 Ndugu Wanahabari Namuomba Mwenyekiti Mh.Rais Dkt. Magufuli aunde Tume ya Uchunguzi wa Mali za Jumuiya ya Umoja wa Vijana kwani Hali yake ni Mbaya Juu ya Mambo yafuatayo.

1. Mapato ya Jengo na Juu ya Matumizi ya Fedha zinazopatikana na Mapato hayo ikiwa ni Mradi mkubwa wa Jumuiya ya Vijana(UVCCM ).

2.Minada Holela ya Mali za Chama ikiwemo Magari n.k.ambayo imekua ikifanyika kinyume na Taratibu.

3.Uuzwaji wa Viwanja(Mashamba) vya Jumuiya Mkoani Iringa.
4.Kushughulikia Wasaliti ndani ya Chama na Jumuiya Yetu ya UVCCM ambao wamekua mchana CCM usiku vyama vya upinzani.

   Namuombea sana Mheshimiwa Rais Wetu ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa kila siku ya Mungu kwani mambo anayofanya kwa Taifa kwa sisi wanyonge tupo Pamoja naye, lakini kuna baadhi ya waliozea njia za Ujanja Ujanja wanamuona kama adui. Endelea Mh.Mwenyekiti Dkt Magufuli  ambao tunakuamini tu Wengi, Tanzania Yetu kwa Muda mchache umeonesha Dhamira yako ya Kutufikisha Tanzania Mpya yenye Uchumi wa Viwanda, Kumiliki ndege zetu, Ukusanyaji madhubuti wa Mapato ya ndani, Kurudisha nidhamu serikalini kwa watumishi wa Umma, Mali za Umma kutoshezewa ovyo, Kufanikisha Elimu Bure, Kufanikisha uundwaji wa Mahakama Maalumu ya Kushughulikia Kesi za Mafisadi , wala Rushwa na Wahuhujumu Uchumi.
    Ndg. James Rock Mwakibinga,

   Kada CCM , mwanachama UVCCM.


          Dodoma, Tanzania