Mzee Mohamed Hamisi Mahoka ‘Mzee Chinga’ Muasisi wa Upinzani Mkuranga

Na Wilson Makubi, Mkuranga
Muasisi wa chama cha Wananchi C.U.F Wilaya ya Mkuranga Mzee Mohamed Hamisi Mahoka , ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kisasa Wilaya ya Mkuranga, maarufu kwa jina la Mzee Chinga amewaasa Vijana wa Wilaya Mkuranga hasa kwa Kata zilizo pembezoni mwa Mji wa Dar es Salaam kuacha kushiriki katika maandamano hayo ambayo hayana tija kwa Chama wala Taifa kwa ujumla'

Akiongea na Vijana Nyumbani Kwake Kitongoji cha Kisasa Kijiji cha Mlamleni Kata ya Tambani Wilaya Mkuranga alisema‘kwamba baadhi ya Wanasiasa wamekosa ajenda za kimaendeleo kwa ajili ya Watanzania, hivyo wana tafuta sababu ya kujijenga kisiasa ili kujipatia umaarufu’’ pia alisisitiza kwamba wao kama Wazee wa Upinzani watafanya siasa za upinzani zenye tija ili kunusuru umma qwa Watanzania na wanamuomba Mh Rais Jonh P. Magufuli ashighulikie kero za Wananchi bila ya woga,kwa sasa sijaona Mtu anayefanana na Magufuli kwa Nafasi ya Uraisi, Yeye anatosha’’
Vijana Niwambie enzi za ukoloni hamkuwepo kiasi kwamba hamjaona vurugu za serikali sasa mnataka kuijaribu serikali yenu, nawashauri Msishiriki jambo msilolijua, Raisi Magufuli amefanikiwa kupambana na hoja ya ufisadi hivyo ambayo ilionekana kuwa ni ngao ya upinzani katika majukwaa, sasa hawana cha kusema wanatafuta sababu nyingine ili wasikike.
Mzee Chinga alimalizia kwa kusema kwamba ‘Ni vyema sasa Wabunge wanaotaka kuandamana wanapokuja majimboni mwetu watuambie wamefanya nini katika muda waliokaa madarakani na sio kututia matatizoni, wajibu wao ni kuleta maendeleo katika majimbo lakini tofauti na wabunge wa Chadema ambao wao lengo kubwa ni kubishana na serikali, hii ni dalili kwamba uwezo wao wa kushughulikia kero za Wananchi ni Mdogo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...