Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anaeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Luahaga Mpina Ametoa wito kwa taasisi za Muungano zinazofanya tafiti za kisayansi, kufanya tafiti hizo ziwe na tija kwa Serikali na Umma.

Mpina aliyassema hayo, alipotembelea taasisi ya Muungano ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha DSM ..iliyopo katika Wilaya ya Magharibi B nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar, iliyopo chini ya Wizara ya Wizara ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya Kukagua jengo jipya la taasisi hilo ambalo halijaanza kutumika ikidaiwa ni kutokana na changamoto mbalimbali pamoja na ukosefu wa samani, Naibu Waziri Mpina aliishauri tafiti za taasisi hiyo ziwe zenye malengo ya kusaidia watanzia wanaoishi katika ukanda wa pwani ili kuwawezesha kusaidia kuinua uchumi wao na kuongeza pato la taifa.

Aidha, Mpina aliongeza kwa kusema kuwa anategemea tafiti zinazofanywa na taasisi hiyo zitoe muongozo kwa serikali na namana ambavyo nchi inavyoweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. “Hakikisheni serikali inapata taarifa zenu ili ziweke kutumika, mpo kimya sana na hamsikiki.” Alisisitiza Mpina.

Kwa upande mwingine taasisi hiyo imekuwa pia ikitoa nafasi kwa wanafunzi wageni toka katika nchi mbali mbali duniani kuja kujifunza na kufanya tafiti juu ya viumbe hai waishio baharini aina ya Pomboo (Dolphin)ili kuweza kufahamu mazingira na tabia za ndani za viumbe hao na kubadilishana uwezo na kuongeza kipato kwa taasisi hiyo kupitia malipo ya mafunzo hayo maalum. Naibu Waziri Mpina pia, alitoa Pongezi kwa taasisi hiyo kuwa na jengo zuri pamoja na changamoto wanazokabilana nazo na kuwashauri wahamie na kuanza kulitumia jengo hilo.

Ziara ya Naibu Waziri Mpina Mjini Zanzibar pamoja na kumuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mhe.Samia Suluhu Hassan katika siku ya Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, inahusisha pia kutembelea baadhi ya taasisi za muungano mjini humo.
Naibu Waziri Ofisi Ya Makamu wa Rais anaeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipata Maelezo toka kwa Dkt. Mohammed Maalim Mtaalam wa Maabara ya Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha DSM ..iliyopo Zanzibar, moja wapo ya taasisi ya Muungano ililopo chini ya Wizara ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Naibu Waziri Mpina Yupo Mjini Zanzibar katika ziara ya kikazi.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, kati kati ni Dkt. Yohana Shebule muhadhiri wa ya Taasisi ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, na Makamu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Profesa Mtolela wakitembea kukagua jengo jipya la taasisi hiyo lililopo Buyu, nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, pamoja na ujumbe wake wakisikiliza taarifa na changamoto za jengo jipya la za Taasisi ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, toka kwa dkt.Yohana Shebuda hayupo pichani, wakati wa kukagua jingo hilo pamoja na kuzungumza na watumishi wa taasisi hiyo.
Katika Picha ya pamoja aliyekaa kati kati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina pamoja na watumishi wa Taasisi ya ya Elimu Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyopo Buyu katika wilaya ya Magharibi B nje kidogo ya mji mkongwe wa Zanzibar. (Picha na Habari zote na Evelyn Mkokoi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...