Wakazi wa kijiji cha Kizimkazi kilichopo katika jimbo la Makunduchi Mkoa wa kusini unguja, wamekuwa na utaratibu wa kuadhimisha siku ya kizimkazi, maarufu kama kizimkazi day ambayo hufanyika kila mwaka mwezi wa nane.

Siku hiyo maarufu katika kijiji hicho ambayo imeanzishwa na aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo la Makunduchi mhe. Samia Suluhu Hassan ambae sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikiadhimishwa kijijini hapo kwa namna ya kipekee ya burudani, mashairi na michezo mbali mbali ambapo pia wana kizimkazi wamekuwa wakipata nafasi ya kuainisha changamoto mbali mbali zinazo wakabili katika kijiji hicho.

Akimuwalisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina amehaidi kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili wakazi wa kijiji hicho kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Makunduchi mhe. Haruna Suleiman ambae pia ni Waziri wa Katiba, Sheria Utumishi wa Umma na Utawala bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuchangia mifuko 100 ya simenti na mabati 100, na matofali 2000 ya kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo vimeanishwa kuwa moja ya changamoto kijijini hapo.

Aidha, amewaahidi wana kizimkazi kuwa kwa kushirikiana na mbunge na uongozi wa serikali uwanja wa mpira ambao umekuwa ukihitaji matengezo nao utaanza kusawazishwa kwa ajili ya michezo kijijini hapo.

Wana Kizimkazi wamebainisha kukabiliana na changamoto itokanayo na mapato na matumizi ya rasilimali ya bahari, pamoja na kupungua kwa nishati ya umeme kutokana na ongezeko la mahitaji litokanalo na mji huo kupanuka.

Kwa upande mwingine Naibu Waziri Mpina Pia alimuwailisha Makamo wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika kampuni inayotengeneza nishati ya mkaa rafiki wa mazingira inayotumia malighafi itoknayo na taka za maganda ya miwa na makarati na kuwapongeza kwa jitihada kubwa za utunzaji wa mazingira kwa kutokukata miti ovyo na ubunifu wa nishati hiyo.

Ziara ya naibu Waziri Mpina Mjini Zanzibar ni Sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Pamoja na kumuwakilisha Mhe, Makamu wa Rais katika siku maalum ya Kizimkazi. Kizimkazi Day.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina aliyevaa suti akishika na kuangalia nishati ya mkaa unaotengenezwa na malighafi itokanayo na taka za miwa na karatasi mjini Unguja, alipomuwakilisha Makamu wa Raisi Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kampuni ya Blue Spot, inayotengeneza nishati hiyo bila kuharibu Mazingira.
Mabinti Mapacha Sabra na Sabrina Hassan wa shule ya sekondari makunduchi wakitumbuiza kwa utenzi kwa meza kuu haipo pichani, wakati wa mkutano wa Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Hayupo pichani, kijijini Kizimkazi wakati wa siku ya kizimkazi ambapo Naibu waziri Mpina alimuwakilisha Mhe. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la makunduchi.
Aliyesimama Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Pamoja na baadhi yaViongozi mbali mbali wa jimbo la Makunduchi mkoa wa kusini Unguja, akizungumza na wanachi (hawapo pichani) wa jimbo hilo katika kijiji cha kizimkazi .katika siku ya kizimkazi maarufu kama kizimkazi day, alipomuwakilisha mhe. Mkamu wa Rais Mama Samia Suhulu Hassan aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...