Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amezitaka Maabara Nchini kuhakikisha zinafuata misingi na kanuni sahihi katika kuzingatia ubora na ufanyaji. 
Akiwa katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Shinyanga, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla aliweza kukagua Maabara ya Hospitali ya Wilaya ya Kishapu ambapo alibaini mambo mbalimbali yakifanywa bila kuzingatia taratibu sahihi za Mabara huku akiagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanarekebisha mapungufu hayo katika Maabara hiyo. 
Miongoni mwa mambo ambayo alikuta katika Maabara hiyo ni pamoja na kutokuwa na taratibu za kiutendaji hasa kwa wafanyakazi wenyewe wa Maabara ambao walishindwa kuzingatia vigezo na msharti ambayo taratibu za Maabara zinahitaji. (Tazama video hapa nchini kuona tukio hilo).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...