Mfalme wa Muziki wa Miondoko ya Pwani (Taarabu) Afrika Mashariki na Kati, Mzee Yusuf leo ametangaza kuachana rasmi na muziki huo wa kidunia na kuamua kumrudia mwenyezi Mungu.

Mzee Yusuf ametangaza hivyo leo Ijumaa Agosti 12, 2016 Muda mfupi baada ya kumaliza swala ya Ijumaa katika msikiti wa Ilala Bungoni (Masjid Taqwa) huku akibubujikwa na machozi mengi.

Mzee Yusuf ameomba waumini wamuombee msamaha kwa Allah kwa kipindi chote alichokuwa amemuasi na kadhalika amewaomba wanamuziki wengine ambao ni waislamu kuachana na muziki na kuzitumia fani zao walizonazo katika kutangaza na kumsifia bwana Mtume Muhammad (s.a.w).

Aidha amewaomba watu wote wenye Cd zake majumbani pamoja na vituo vya redio na televisheni kuacha kupiga nyimbo zake na wakikaidi wafahamu madhambi yote yatakuwa juu yao kwani yeye hivi sasa anafanya toba Kwa Allah.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kweli unatakiwa ufanye TOBA ya kweli ya kutokurudia tens.

    ReplyDelete
  2. ALLAHU AKBAR...Masha Allah...JAZAQALLAHU KHAYR...In Sha Allah, Mwenyeez Mungu akughufirie kwa yote uliyopitukia mipaka huko nyuma ulikotokea na In Sha Allah, akulinde na akuongoze katika mambo yote yenye kheri na akujaaliye TOBA YA KWELI na uwe mfano kwa umma wote ili na wengine weweze kuongoka mithli yako na kuifata iliyo ya haqqi "Swiratwal Mustaqeem' kama ulivyoamuwa wewe. Mbele ya ALLAH hakuna lishindikanalo. Na waja sote tu wingi wa makosa, lakini tumeambiwa mbora wao ni yule alibainie kosa lake na akalilia maghufira na kurejea kwa Mola wake ili amsameh na hili na hata miongoni mwetu mara tunapokoseana basi ni wajibu kuombana msamaha na kumuomba MOLA wetu atusameh duniani mpaka kesho akhera na kuwa ni wenye kutubu kwake Toba iliyo ya kweli na hata ibapobidi au kulazimu, basi ni vizuri kujitowa 'Fi Sabili Llah' katika mambo ya kheri yampendezayo Mwenyeez Mungu na kuyaepuka yote yaliyo machukizo na makatazo yake. Nakuombea kila DUA njema MZEE YUSUF kwa uamuzi ulioufanya kwani Dunia ni mapito na Akhera ndio maishilizio yetu. Hivyo tusijisahau tukaghilibika na Dunia na kuisahau kesho Akhera.

    ReplyDelete
  3. sio kuacha muziki tu. na mapato yote yaliyotokana na huo music awapatie maskini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...