THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

NEWS ALERT: TUNDU LISSU AACHIWA KWA DHAMANA

                                              Na Mwene Saidi wa  
                                                 Globu ya Jamii
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu  (pichani) ambaye leo amefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam na kupandishwa kizimbani dhidi ya mashtaka matatu ikiwamo kuidharau mahakama na kusababisha chuki kwa watanzania dhidi ya Rais John Magufuli na serikali yake ameachiwa kwa dhamana.
Lissu alipandishwa kizimbani  na kusomewa mashtaka matatu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Cyprian Mkeha, katika kesi iliyoanza saa 9.26 mchana hadi saa 2.25 usiku. 
Hakimu alitupilia mbali kiapo cha Jamhuri cha pingamizi la dhamana kwa kuwa hakikuonesha tarehe iliyotolewa. 
Kisha Hakimu akamtaka mshtakiwa kujidhamini mwenyewe kwa kusaini hati ya dhamana ya shilingi milioni 10. Akafanya hivyona kuachiwa.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi, akisaidiana na Wakili Serikali Mwandamizi Mutalemwa Kishenyi, Mawakili wa Serikali Simon Wankyo na Paul Kadushi.

Wakili Kadushi alidai kuwa Agost 2,2016 akiwa na nia ya kujenga chuki dhidi ya Rais Dk John Magufuli kwamba ni dikteta uchwara. 

Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa siku na eneo la tukio la kwanza mshtakiwa akiwa na nia ya kuleta dharau katika mfumo wa mahakama nchini alitamka kwam a "Kesi    ya kipuuzi na mashtaka yamekaa kimagufuligufuli "alinukuliwa mshtakiwa.
Shitaka la tatu linadai kuwa siku na eneo la tukio la kwanza mshtakiwa baada ya kutoka kusikiliza kesi zake mbili tofauti zinazomkabili katika mahakama hiyo akiwa na lengo la kudharau mahakama alitamka "Siwezi kufungwa mashtaka yenyewe ya kipuuzi yamekaa kimagufuligufuli" alinukuu Wakili Kadushi.
Lissu alidai kuwa maneno anayodaiwa kuyatamka katika hati ya mashtaka ni ya kweli lakini siyo ya uchochezi hivyo alikana mashtaka hayo.
Hata hivyo Wakili Nchimbi alidai kuwa upande waJamhuri unapinga dhamana dhidi ya mshtakiwa kupitia hati ya kiapo iliyowasilishwa na Mkuu wa upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala ( RCO) kwamba mshtakiwa akipewa dhamana atarudia kufanya makosa hayo kinyume cha sheria.
Pia Wakili Nchimbi aliwasilisha pingamizi la kumkataa wakili kiongozi wa utetezi Peter Kibatala kwamba ametoa maelezo polisi na kwamba anatarajiwa kuwa shahidi wa Jamhuri dhidi ya mshtakiwa.
kuhusu uwakili Kibatala alidai kuwa hakuna sheria inayomzuia kumtetea mteja wake na kwamba ni njama za upande wa Jamhuri kwa kuwa wanamhofia.
Kutokana na pingamizi la dhamana, Lissu alilazimika kujibu hoja mwenyewe baada ya upande wa Jamhuri kusisitiza kwamba Kibatala haruhusiwi kumtetea mshtakiwa hadi mahakama itakapoamua vinginevyo.
Alidai kuwa hoja za Jamhuri hazina mashiko ya kuzuia dhamana yake kwa kuwa hajatiwa hatiani na kwamba chini ya kifungu cha 148 kidogo cha (5)a hakijaanisha sababu zilizotolewa na Jamhuri kuzuia dhamana yake.


Kuna Maoni 7 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Tundu Lissu alitakiwa kupuuzwa. Lakini ameandamwaaaa weeee mpaka habari zake imebidi zitoke ktk blogi yetu ya jamii.

 2. Anonymous Anasema:

  Kwa nini apuuzwe?..mashtaka ya Kimagufuligufuli mnamlimbikizia mnafikiri sheria za ni Mali yenu?..Magufuli anatafuta balaa Tanzania siyo Rwanda wala Uganda..atafunga wangapi? Huu ni wazimu..

 3. Obama Anasema:

  Tuache demokrasia Itawale

 4. Anonymous Anasema:

  Mara athari za uchochezi zitakapo likumba taifa si Lisu au wewe utakuwa salama. Ifike mahali watu waweze kutambua,kuheshimu sheria za nchi.Inawezekana kabisa kufanya siasa bila kutoa kashfa, au maneno ya kudhalilisha watu wengine.Jiulize,mbona Msigwa alihutubia on the same day na hakukamatwa?

 5. Nini chanzo Anasema:

  Haya yote yanatokea wapi?...

 6. Anonymous Anasema:

  Hawa akina Lissu fujo ndio chakula yao.wengine tusidanganywe