THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

NGOMA AFRICA BAND KUTUMBUIZA LEO JUMAMOSI 13 August 2016 FRANKFURT,UJERUMANI

Na Zainab Ally Hamis, (DSJ)

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya, Ngoma Africa Band yenye makao yake kule Ujerumani, wanatarajiwa kutingisha jukwaa katika maonyesho ya Afrika-Karibik Festival litakalo fanyika jumamosi hii 13 August 2016 katika viwanja vya Rebstock Park,jijini Frankfurt,Ujerumani, ambapo wapenzi wa muziki watapata burani ya aina yake kutoka kwa bendi hiyo iliyofanikiwa kuwanasa washabiki kila kona duniani.

Kikosi cha Ngoma Africa band kinachoongozwa na mkuu wake mwanamuziki Ebrahim Makunja a.k.a Kamanda ras Makunja mkuu wa viumbe wa ajabu (Anunnaki Aliens) kinadumu katika gemu la muziki kwa takribani miaka 23 sasa na kuwekwa katika rekodi ya kimataifa kuwa ndio bendi ya kiafrika inayodumu kwa muda mrefu barani ulaya.

usikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com