Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band maarufu kama FFU-Ughaibuni inayoongozwa na mwanamuziki nguli Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja juzi kati ya jumamosi ya 13 Septemba 2016 ilifanikiwa tena kulitingisha jiji la Frankfurt nchini ujerumani katika maonyesho ya Afrika-Karibik Festival yaliyo fanyika katika viwanja vya Rebstock Park,ambapo bendi hiyo iliwatia kiwewe waudhuriaji wa onyesho hilo.
Bendi hiyo maarufu na mdundo wake "Bongo Dansi" inatajwa kuwa ndio bendi imara ya kiafrika kudumu kwa muda mrefu na kuteka soko la muziki barani ulaya.
 Ngoma Africa band wakishambulia jukwaa jijini Frankfurt
 Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja akiongoza gwaride la FFU Ughaibuni
 Mashabiki wa kila rika na rangi walipata kiwewe kila dakika ngoma zikipigwa
 Palikuwa hapatoshi
Kiongozi wa Ngoma Africa Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja akizongwa na mashabiki baada ya gwaride kali la FFU Ughaibuni jijini Frankfurt 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. FFU-Ughaibuni chini ya kamanda mti mkavu Ras makunja kiongozi wa viumbe wa ajabu Anunnaki aliens si mchezo

    ReplyDelete
  2. Watoto wa mbwa aka ngoma afrika band wasio pingika kila kona mnatesa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...