Kaimu Afisa Mkuu Wateja Binafi wa  NMB, Boma Raballa akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa kukabidhiana Mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa Waandaaji wa Mashindano ya Rock City Marathon kwa mwaka 2016 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Afisa Mkuu Wateja Binafi wa  NMB, Boma Raballa pamoja na Mratibu wa Mashindano ya Rock City Marathon, Mathew Kasonta wakikabidhiana Mfano wa Hundi yenye thamani shilingi milioni kumi kwa ajili ya maandalizi ya Mashindano ya Rock City Marathon kwa Kampuni ya Capital Plus International Ltd anaeshuhudia nyuma ni Msimamizi Mkuu wa Kampuni hiyo ya Capital Plus, Erasto Kilawe.
Mratibu wa Mashindano ya Rock City Marathon, Mathew Kasonta akizungumzia juu ya maandalizi waliyoyafanya katika mashindano ya Rock City Marathon kwa mwaka 2016. 

BENKI ya NMB imeipiga jeki Kampuni ya Capital Plus Ltd kwa kuikabidhi Mfano wa Hundi wenye thamani ya shilingi milioni kumi kuandaa Mashindano ya Rock City Marathon kwa mwaka 2016.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhiana Mfano wa hundi hiyo,Kaimu Afisa Mkuu Wateja Binafsi wa Benki hiyo, Boma Raballa amesema wamefarijika na wameamua mara moja kushirikiana na Kampuni hiyo ya Capital ili kuwa chachu ya maendeleo ya Michezo kwa jamii nzima ya Tanzania.

"Tunashukuru pia kwa kutambua kuwa NMB ni mahala sahihi pa kukimbilia, hii inaonesha kuthamini kwenu mchango wetu kama benki katika kuchangia maendeleo" amesema Raballa

Amesema kwa miaka kadhaa sasa NMB katika mipango yake imekuwa ikishiriki shughuli mbalimbali za kijamii kama kusaidia sekta ya elimu kutoa mchango wa Madawati na Viti. Afya na pia kufariji jamii katika vipindi vya majanga mbalimbali kama mafuriko na ajali mbalimbali.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mashindano Kampuni ya Capital Plus,Mathew Kasota amesema mbio hizo zinafanyika kwa mara ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009 zikiwa na lengo la kisaidia utambuzi, uhamasishaji na uibuaji wa vipaji vya riadhi nchini

Amesema Rock City Marathon zinahusisha makundi matano yaani mbio za kilomita 21 kwa wanaume na wanawake,kilomita 5 kwa ngazi ya 'corporate', kilomita 3 kwa ajili ya walemavu na zile za wazee umri zaidi ya miaka 55 na kuendelea pamoja na kilomita 2 kwa ajili ya watoto umri kati ya miaka 7 hadi 19.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 25 mwezi wa tisa huko Mkoani Mwanza. Fomu zinapatikana jijini Mwanza na mikoa jirani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...