Benki ya NMB imeendelea kutanua mtandao wa matawi yake nchini ili kuwa karibu zaidi na wateja wake. Mwishoni mwa wiki iliyopita, NMB ilizindua tawi jipya la NMB Rock City lililopo ndani ya jengo jipya la kibiashara la Rock City jijini Mwanza.

Tawi hili linafanya jumla ya matawi ya NMB kwa Mwanza mjini kufikia matano na 28 kwa kanda nzima ya ziwa ni imani ya NMB zinduzi huu unaleta tumaini jipya kwa wateja wa NMB jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla. Huduma zinazotolewa na tawi hili jipya ni pamoja na kufungua akaunti, mikopo, huduma ya fedha za kigeni, huduma za kuweka na kutoa fedha.

Katika kuhakikisha kuwa NMB inahudumia makundi mbalimbali ya wateja wake kulingana na mahitaji yao ya kifedha, wiki iliyopita, benki iliendesha mkutano wa Klabu ya Biashara uliowakutanisha pamoja zaidi ya wateja 300 wanaohudumiwa na matawi ya NMB ya jijini Mwanza. Baadhi ya faida zilizopatikana katika mkutano huo ni pamoja na mafunzo ya jinsi ya kukuza biashara, elimu ya mlipa kodi, jinsi ya kutunza daftari la biashara na njia mbalimbali za kuboresha biashara.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela (katikati) akikata utepe kuzindua tawi la Rock City Mall la benki ya NMB jijini Mwanza, wa tatu kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NMB Bi Magreth Ikongo na wa tano kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Ineke Bussemaker.
Meneja wa NMB kanda ya ziwa- Abraham Augustino akiongea katika mkutano wa klabu ya biashara uliofanyika jijini Mwanza wiki iliyopita. Zaidi ya wateja 300 walihudhuria mkutano huo ambapo pamija na mambo mengine walipata mafunzo ya jinisi ya kukuza biashara, elimu ya mlipa kodi na njia mbalimbali za kuboresha biashara.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurungezi ya NMB- Margaret Ikongo akizungumza katika mkutano wa Klabu ya Biashara jijini Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...