THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

PROF. MBARAWA AZUNGUMZA NA WADAU WA MAENDELEO.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza mjumbe wa wadau wa maendeleo katika kikao kazi kujadili namna ya kushirikiana katika ujenzi wa miundombinu ya kisasa nchini, kikao hicho kimefanyika Jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji na Tathmini (Sekta ya Uchukuzi), Bw. Aunyisa Meena akifafanua jambo katika kikao kazi kujadili namna ya kushirikiana katika ujenzi wa miundombinu ya kisasa baina ya viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na wadau wa maendeleo, Jijini Dar es salaam.
 Wadau wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia (WB), Umoja wa Ulaya (EU), Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na  Shirika la Maendeleo la Japani (JICA) wakisikiliza maelezo ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) kuhusu mikakati ya Serikali kuimarisha miundombinu na kukuza uchumi katika kikao cha pamoja kilichofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa  wadau wa maendeleo katika kikao kazi kujadili namna ya kushirikiana katika ujenzi wa miundombinu ya kisasa nchini, kikao hicho kimefanyika Jijini Dar es salaam.
Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (W-UUM).

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewahakikishia wadau wa Maendeleo kuwa Serikali ya Awamu ya Tano iko tayari kupokea changamoto na ushauri utakaoiwezesha kutimiza adhma yake ya kuwa na miundombinu bora na yakisasa itakayoiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya wataalam wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na wadau wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia (WB), Umoja wa Ulaya (EU), Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na  Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), Prof. Mbarawa amewahakikishia wadau hao wa maendeleo kuwa wizara yake inatarajia ushirikiano mkubwa hususani katika sekta ya ujenzi wa reli, barabara, bandari na viwanja vya ndege.

“Sekta ya Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano inachukua asilimia kubwa ya bajeti ya nchi yetu hivyo licha ya jitihada na misaada mnayotupa bado tupo tayari kupokea misaada, changamoto na ushauri ili ituwezeshe kukamilisha kwa wakati na ubora miradi ya ujenzi inayoendelea na tunayotarajia kuianzisha”, amesema Prof. Mbarawa.

Profesa Mbarawa amesisitiza kwamba Serikali imejipanga kudhibiti rushwa ili fedha nyingi zinazotumika katika miundombinu ilete matokeo chanya na kuwahakikishia kwamba ujenzi wa reli ya kisasa ya kati (Standard Gauge), itaanza baadaye mwaka huu na ikikamilika itapunguza gharama kubwa za usafirishaji zinazotumika kupitia malori.

Profesa Mbarawa amewashukuru wadau wa maendeleo kwa misaada mbalimbali wanayotoa katika sekta ya ujenzi wa barabara na ukarabati wa reli mara kwa mara na kusisitiza kwamba Serikali inatambua na kuthamini michango hiyo na kuomba washirikiane katika ujenzi wa reli ya kisasa ya kati (Standard gauge).

Zaidi ya kilomita 2600 za Reli ya Kisasa (Standard gauge) zinatarajiwa kujengwa kutoka Dar es Salaam-Morogoro-Dodoma-Tabora-Isaka hadi Mwanza ambayo ni uti wa mgongo wa reli hiyo. 

Na Sehemu nyingine ni kutoka Tabora-Mpanda hadi Kalemela na Tabora-Uvinza hadi Kigoma ambayo itaunganisha na nchi za Rwanda na Burundi na hivyo kufungua huduma za kiuchumi na uchukuzi kati ya Tanzania na nchi za maziwa makuu.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano