Na Daudi Manongi, MAELEZO.
MWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii Prof Samwel Mwita Wangwe amesema kuwa uongozi wa Awamu ya Tano umefanya kazi kubwa katika kuweka maslahi ya Taifa mbele ikiwamo kuongezeka kwa bajeti ya maendeleo na kupunguza matumizi ya serikali.

Hatua hii imesaidia nchi kusonga mbele kupitia uboreshaji wa  utendaji kwa watumishi wa umma na hivyo kujenga imani kubwa kwa wananchi juu ya Serikali yao.

Profesa Wangwe ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akitoa tathmini ya uongozi wa Awamu ya Tano.

Amesema kuwa Rais Magufuli katika uongozi wake umesaidia  kuokoa fedha nyingi za walipa kodi ambazo zilikuwa zikiishia mikononi mwa watu wachache na kuzielekeza katika shughuli nyingine za maendeleo.

Profesa Wangwe amewataka wananachi kumuunga mkono Rais Magufuli kwenye harakati zake za kupambana na matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuwa matokeo yake yatasaidia kuijenga Tanzania mpya ambayo kila mwananchi atapata fursa kunufaika na rasilimali za nchi.

“Kwa kweli Rais huyu amefanya mabadiliko makubwa sana na kwa sasa  nchi imerudi katika hali  nzuri,  kwani nchi ilikuwa imefika mahali pabaya na kwa hiyo aliona ni budi kuhakikisha Rushwa na Ufisadi vinakomeshwa na kwa hili ameanza vizuri na nchi inakwenda katika mwongozo mzuri kwani ameboresha utendaji kazini serikalini na kubana matumizi ambayo yamesaidia kuokoa pesa nyingi ambayo inatumika katika maendeleo ya nchi hii”aliongeza Profesa Wangwe.

Mbali na hayo Profesa Wangwe ameshauri Serikali kuweka mfumo mzuri katika ukusanyaji kodi kwa kurasimisha biashara ili mfumo huu wa  EFD utumike kirahisi na pia kutengenezwe mazingira mazuri ya biashara kwa kuweka mazingira rahisi ya kuandikisha biashara kwani huchukua muda mrefu kwani kwa kufanya hivyo kasi ya kurahisisha  utendaji na wafanyabiashara watalipa kodi kwa wingi na uchumi utakua.

Pia Profesa Wangwe ametoa ushauri kwa vyama vya upinzani kuacha na na maandamano yasiyo na tija na badala yake wakae chini na kuzungumza na serikali ilikupata mwafaka na hivyo amani iendelee kuchanua katika nchi hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. MHE PROFESOR WANGWE KWA KWELI TUNASIKITIKA SANA TULICHOFANYIWA NA SERIKALI HII YA AWAMU YA TANO,LAKINI HUENDA RAIS KAAMBIWA SIVYO,NA WAZIRI WAKE WA MALIASILI NA UTALII KIASI INAUMA UKWELI NI KUWA TUMEINGIZWA KWENYE UMASIKINI AMBAO HATA AMBAO HATIKUWA NAO KIASI TUNAONA HII SERIKALI IMETUUA.UKWELI NI HUU WAFANYABIASHARA YA VIUMBE HAI NA WENYE MASHAMBA TULICHOFANYIWA NI KIBAYA SANA TUMEKATA LESENI ZETU KAMA KAWAIDA ZA MWAKA HUU 2016,KUANZIA JANUARY -HADI DECEMBER 31,2016.TUMELIPIA WANYAMA,NDEGE,NA MIJUSI NK,WATU WAMELIPIA PERMITS ZA KUKAMATA NA KUFANYA EXPORT LAKINI WAZIRI BILA KUJALI NINI TUNACHO AU GHARAMA TULIZONGIA AMETANGAZA KUFUNGA BIASHARA HII TANGU MWEZI MARCH 2016 HADI LEO.TUNAUGULIA UMASIKINI WA KUTISHA,MADENI,GHARAMA ZA KUTUNZA ,KULISHA,VIFO,TUNA QUOTA HALALI ZA MWAKA 2016 TUNA VIUMBE HAI,MIKOPO YA MABENKI,NI HUZUNI KUSEMA KUWA TUMEINGIZWA KWENYE LINDI LA UMASIKINI WA KUTISHA,JE MHESHIMIWA WANGWE UTAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI KWA HALI HII?????? JE HAWA WANYAMA AMBAO WAKO KWENYE MASHAMBA AMBAO INVESTMENT KUBWA ZIMEFANYWA NANI ATALIPA HASARA HII.UUNGWANA UMETUSHINDA HATA MUNGU AMEONA UVUMILIFU UMETUSHINDA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...