Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
WAZIRI wa Elimu , Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameiagiza Mamlaka ya Elimu Ufundi, Stadi (VETA) kuhakikisha vyuo vyote vya VETA vinakuwa na ubora sawa katika kuwafanya vijana kuajirika au kujiajiri wenyewe.

Profesa Ndalichako ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Chuo cha Ufundi Stadi cha Kipawa, amesema kuwa hata VETA ndio wasimamizi wa vyuo vya ufundi kuhakikisha wanazalisha vijana wenye uwezo sawa na sio kutofautiana na kufanya wananchi kuhangaika katika vyuo,Amesema vijana wakipata mafunzo yenye ubora kutafanya vijana kuacha kuhangaika na vyeti kwa ajili ya kutafuta kazi hiyo inatokana na kuwa na uwezo binafsi wa kujiajiri au kuunda kampuni na kuweza kuajiri wengine.

Amesema kuwa kuna sehemu ya vyuo ametembelea na kukuta kuna changamoto ambazo kama menejimenti ya VETA kuhakikisha wanafanyia kazi changamoto hizo ikiwemo kuwa na mitambo ya zamani hali ambayo inafanya vijana kushindwa kupata kile ambacho kinahitajika katika kuelekea uchumi wa viwanda.

Profesa Ndalichako amesema mafunzo ya VETA yawe ya kisasa na maeneo mengi ambayo inamilki haitumiki na kutaka kubadili mtazamo wa uendeshaji katika kuendana na adhima ya serikali.
aidha ameitaka VETA kufanya tathimini ndani ya mwezi mmoja na wapeleke ripoti hiyo juu ya uendeshaji ikiwemo changamoto zinazowakabili .

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA , Geoffrey Sabuni amesema chuo cha Kipawa ni maalumu kwa ajili ya ICT na kufanya vijana wanaozalishwa kuwa na utalaamu ambao unafanya waweze kujiajiri au kuajiriwa na wakitoka katika chuo hicho huwawarudi.

Amesema kuwa wamejipanga katika utoaji wa mafunzo katika kuweza vijana kuingia katika uchumi wa viwanda wakiwa ndio wataalamu wenye uwezo wa kutosha katika sekta hiyo.




mwalimu wa Ufundi Ricky akionyesha baadhi ya mashine zinazotumika kufundishia wanafuinzi wanaojiunga na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Kipawa.

Picha ya pamoja kayi ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akiwa na watendaji wa Chuo cha VETA Kipawa pamoja na baadhi ya wanafunzi chuoni hapo
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)juu ya mikakati ya Serikali kuelekea Uchumi wa Viwanda ambapo chuo cha VETA Kipawa inajikita zaidi kutoa mafunzo yanayohusu masuala ya viwanda.

mmoja wa wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Mlimani waliokwenda chuoni hapo kupata mafunzo kwa vitendo juu ya masuala ya TEHAMA .picha na Beatrice Lyimo-MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...