RAIA wawili wa Kigeni wakamatwa jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuishi hapa nchini bila kibali na kuwa watumishi wa Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam John Msumule amesema kuwa  Raia hao ni Bw.Bahilanya Milingita maarufu kwa jina la Roy Bilingita raia wa Congo  na Dkt. Esther Green Simon Mwenitumba raia wa Malawi.

Amesema kuwa Bw.Bahilanya Milingita maarufu kwa jina la Roy Bilingita raia wa Congo ambaye anatuhumiwa kuingia nchini mwaka 1986 na kufanya kazi katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  kinyume na sheria za nchi, na Dkt. Esther Green Simon Mwenitumba raia wa Malawi ambaye alikuwa Mganga Mkuu katika kituo cha Afya Mburahati anatuhumiwa kufanya kazi Serikalini wakati si raia wa Tanzania.
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam John Msumule akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watumishi wawili wa Serikali ambao sio raia wa Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Watuhumiwa ambao sio raia wa Tanzania waliokuwa wakifanya kazi serikalini wakiwa chini ya ulinzi wa askari wa Uhamiaji, kushoto ni Bw. Bahilanya Milingita aliyekuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)na kulia ni Dkt. Esther Green Simon Mwenitumba ambaye alikuwa Mganga Mkuu Kituo cha Afya Mburahati.
Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Wapewe uraia hao uzembe wa serikali. Nadhani wanastahili uraia tusiwaonee bure tena cha ajabu zaidi kufanya kazi serikalini. Nadhani Tanzania serikali yetu ililala usingizi wa pono kwa muda Mrefu.

    ReplyDelete
  2. kama ni wamekolifai kwenye taaluma zao ufanyike utaratibu wa kuwapa vibali waendelee kutimikia nchini. Ni gharama kubwa sana kusomesha daktari au mhandisi.

    ReplyDelete
  3. Kama wanajua kiswahili vzr waendelee tu na kazi,na kama utendaji wao kzn pia ni mzuri hatuna aja ya kuwatumbua.

    ReplyDelete
  4. Wsamehewe tu na wapewe uraia kama wapo tayari kubadili uraia wao

    ReplyDelete
  5. Wasamehewe tu

    ReplyDelete
  6. Tanzania bwana in balaa mtaka kumtimua daktari. Sawa bwana

    ReplyDelete
  7. Waachieni wachape kazi wachangie maendeleo ya nchi. Waulizwe tu kama wanataka uraia- wakisema hapana basi warudishwe kwao.

    ReplyDelete
  8. Lakini kwa nini walidanganya? Hilo ndio kosa Lao, lazima waadhibiwe kwa udanganyifu huo, na wapo wengi tu wanaofanya kazi bila vibali Tanzania serikali ya awamu ya 5 endeleeni kuwasaka mtashangaa nchi ilikuwa haina mwenyewe! Asante Mungu kwa kutuletea kiongozi wa kweli mwenye uchungu na nchi!! "MUNGU IBARIKI TANZANIAN"

    ReplyDelete
  9. Hao inabidi wapate uraia kwa vile wamekaa mda mrefu na ni asset kwa nchi

    ReplyDelete
  10. Kaaaazi kwelikweli.....

    ReplyDelete
  11. Hawa wapewe uraia huu ulikuwa uzembe wa serikali. Wametoa huduma muda mrefu kwa serikali. Kama wana makoasa ya jinai basi warudishwe. Home is where your heart is. Hawa wanaomekana hapa Tanzania ni kwao. Bwana Michuzi peleka hili kwa Magufuli wapewe citizenship based on humanitarian grounds. Hata Obama anampango wa kuwasemehe wahamiaji wengi haramu. Serikali please BE HUMAN!

    ReplyDelete
  12. Wapewe uraia na waendelee na kazi kwa manufaa yetu wenyewe.

    ReplyDelete
  13. Wapewe uraia waendelee na kazi kwa manufaa yetu wenyewe.

    ReplyDelete
  14. Uingereza ukikaa KINYEMELA miaka 10 mfululizo bila kushikwa basi UNA HAKI YA KUPEWA URAI WA UINGEREZA. Common sense, me thinks!

    ReplyDelete
  15. The mdudu, wengi wenu wote mmechemka eti wapewe uraia why? fanyeni haraka sana wafungwe nyundo 50 na waludishe pesa zetu zote ili ziende kwa watoto yatima hilo nikosa la jinai washa vujisha siri nyingi sana za nchi yetu na itakua walikua wanawaambia wezao njooni Tanzania ni shamba la bibi so acheni wakione cha mtama kuni toka kwa JPM. ili liwe fundisho kwa washenzi kama hao

    ReplyDelete
  16. hii kitu ina hadidhi yumba yake, huyo bibie ni aunt yangu kabisa, so b4 kuongea USENGE, jua nn unaongea cio unafunguka tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...