Kaimu Mnyikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimsalimia  Bw. Thomas Kone (35) akiwa makao makuu ya TBC 1 alikuoitwa kukabidhiwa   Bajaji yake mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alimuona kwneye kipindi cha TV   katika TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji TAnzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba ambaye mwanahabari wake Mbozi Katala ndiye aliyemtangaza bwana Kone.

 Kaimu Mnikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimkabidhi funguo na nyaraka Bw. Thomas Kone (35) kwa ajili ya Bajaji mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kumuona katika TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji TAnzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba ambaye mwanahabari wake Mbozi Katala ndiye aliyemtangaza bwana Kone. Hafla hii fupi imafanyika makao makuu ya TBC 1 Mikocheni jijini Dar es salaam leo Agosti 18, 2016
 Kaimu Mnyikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimwangalia Bw. Thomas Kone (35) akipanda  Bajaji yake mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alimuona kwneye kipindi cha TV   katika TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba ambaye mwanahabari wake Mbozi Katala ndiye aliyemtangaza bwana Kone. Hafla hii fupi imafanyika makao makuu ya TBC 1 Mikocheni jijini Dar es salaam leo Agosti 18, 2016
 Kaimu Mnyikulu ambaye pia ni Naibu Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike akimwangalia Bw. Thomas Kone (35) akiujaribu  Bajaji yake mpya ambayo amezawadiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alimuona kwneye kipindi cha TV   katika TBC1 akiwa anatafuta msaada wa usafiri ili aweze kujikimu kimaisha na familia yake ya mke na watoto wawili. Rais aliguswa na kijana huyu na kuamua kumsaidia kwani pamoja na ulemavu wake ameendelea kuchapa kazi bila wasiwasi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji TAnzania (TBC) Dkt Ayoub Rioba ambaye mwanahabari wake Mbozi Katala ndiye aliyemtangaza bwana Kone. Hafla hii fupi imafanyika makao makuu ya TBC 1 Mikocheni jijini Dar es salaam leo Agosti 18, 2016.

Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ni kweli kama ulivyosema Bw. Thomas Kone, Mwenyeez Mungu akikunyima miguu sio kuwa kakunyima na vingine, bado kakupa akili, macho na mikono ili uweze kujishughulisha katika kutarazaki na maisha ya kila siku. Juu ya hilo binafsi nakupongeza sana kwa juhudi na jitihada zako za kujituma bila kuchukulia hali yako ya ulemavu kama chambo cha kutojishughulisha na chochote au lolote lile na badala yake umekuwa ni mfano bora na wa kuigwa. Pia pongezi za dhati kwa Mh. Rais wetu Bw. John Pombe Joseph MAGUFULI kwa kuliona hilo na kuguswa nalo na kwa moyo wake wa huruma, imani na upendo nae kaweza kujitolea na kuchangia alijchojaaliwa ambacho pia ndicho kilikuwa kilio chake kikubwa Bw. Thomas Kone ambacho ni kupatiwa 'Bajaji'. Mwenyeez Mungu akuongezee Saba wa Sabini katika kipato chako Mh. Rais wetu na kesho mble ya haki Jaza yako njema utakwenda kuikuta In Sha Allah.

    Ila pia nimehuzunika kidogo kuona hao mabwana hapo (Picha ya kwanza juu) alau wangejivuta pembeni kidogo ndio wakampokea na kumsalimia Bw. Thomas Kone, kuliko hiyo sehemu alipokalia mana pana hiyo alama ya baka hapo alipokaa ila sina hakika kama ni maji au mafuta halafu ndio wanahabari nao wakampigia picha hapo hapo, lakini kwa vile nimeangalia na hii video clip nimepata picha halisi, ila next time wapiga picha wetu muwe mnakaguwa na kuchunguza mazingira mnayochukulia picha zenu ili kuondowa vitendawili visivyo na majibu kwa wasomaji wenu na ku present mandhari nzuri kuendana na picha husika. (hayo ni maoni yangu tu kama nimeelweka).

    ReplyDelete
  2. Big up Mr Presudent kwa moyo wa kuwajali watu wako

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Mh Rais kwa moyo huo na Hongera sana Ndugu yetu Kone kwa juhudi zako..

    Lakini kuna swali la kujiuliza:-Je kuna walemavu wangapi nchini wa aina hiyo wanaoonyesha kuhudi za dhati kabisa katika kukabiliana na mahitaji ya maisha? Na Je wote wakijitokeza pia watasaidiwa Bajaj na Mh Rais kama ilivyokuwa kwa ndugu Kone?

    Maana yangu ni kuwa: Rais ana dhamana pana zaidi sana, msaada wake unapaswa kuigusa jamii yote na nchi nzima. Kumsaidia hivyo ni sawa na Abarikiwe sana kwa hilo, lakini ni vema zaidi ukawepo mpango wa kuwabaini walemavu wanaofanya jitihada nchi nzima, wakaundiwa utaratibu wa kuwawezesha katika maeneo yao ya kazi/makazi kulingana na uwezo walio nao, hii itakuwa na maana kubwa zaidi badala ya kusaidia mtu mmoja mmoja na wengine waliopo maeneo ya vijijini, pengine hata wenye juhudi zaidi ya ndugu Kone wakibakia katika hali ya sintofahamu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...