Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 24 Agosti, 2016 amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Modestus Francis Kipilimba alikuwa Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Dkt. Modestus Francis Kipilimba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Rashid
Othman ambaye amestaafu.
Dkt. Modestus Francis Kipilimba ataapishwa leo mchana tarehe 24 Agosti, 2016
Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Bw. Robert Msalika kuwa Naibu Mkurugenzi
Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Robert Msalika alikuwa Afisa Ubalozi katika Ubalozi wa
Tanzania nchini Ethiopia.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Idara ya Usalama wa Taifa Bw. George Madafa kuwa Balozi na nchi
atakayopangiwa, itatajwa baadaye.
Wakurugenzi na Naibu Wakurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa waliopo
wanaendelea na nafasi zao.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
24 Agosti, 2016
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...