THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

RAIS DKT.MAGUFULI ANA NIA NJEMA KWA WATANZANIA,TUMUUNGE MKONO-MBUNGE WA MKURANGA

Mbunge wa Jimbo la Mkuranga wilayani Pwani Abdallah Ulega amewaondoa hofu wananchi wake na kuwaeleza kuwa wasiwe na wasiwasi kwani Rais Dkt.Magufuli ana nia njema kwa watanzania
 
Mh.Ulega ametoa kauli hiyo wilayani Mkuranga katika mkutano wake wa kuwashukuru wananchi wa kijiji cha Sotele kilichopo kata ya Dondo wilayani humo. Amesema kuwa hakuna haja ya kumchukia Rais kwani anayoyafanya Rais leo yamesababishwa na watu wachache ambao Kazi yao ilikuwa ni kujijali wenyewe tu na si vinginevyo na pia waliwasahau wananchi kuzisikiliza shida na kero zao na kuzifanyia kazi.
 
."Mnajuwa Rais anadhamira ya dhati kabisa na watanzania na katika bajeti ya mwaka huu ndio maana ametenga  fedha nyingi ambazo zimeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi hivyo kinachotakiwa ni kumuunga mkono na kuzidi kumuombea tu"amesema Ulega.
 
Akizungumzia maendeleo ya jimbo la Mkuranga alisema amejipanga kikamilifu kuwaletea maendeleo wananchi wake na ndio.maana anapita kuwashukuru na kuhimiza maendeleo. 

Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibewa kilichopo kata ya Dondo mkoani Pwani ,ambapo katika mkutano huo Mh.Ulega aliwashukuru wananchi hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wao na kisha akatumia fursa hiyo kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi .

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya mkuranga Juma Abed akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Kijiji cha kibewa ambao aliwataka kumtumia mbunge wao Ulega na kwamba ni muda wao sasa kumbebesha majukumu yao kwani ndio kazi waliyompa,na zaidi kuacha siasa na kujikita kufanya kazi.

Badhi ya Wananchi wakifuatilia mkutano wa Mbunge wa jimbo la MKuranga,Mh Ulega alipofanya ziara fupi katika kijiji cha Kibewa Kata ya Dondo katika ziara ya kushukuru kwa wananchi wake baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Mzee aliyejitambulisha kwa jina la Jumbe Kazenga wa kijiji cha Kibewa Kata  ya Dondo akitoa ya moyoni kwake kwa mbunge wa Jimbo la mkuranga Abdallah ulega ambapo pamoja na mambo mengine alimpongeza kwa kazi nzuri aliyoianza,ulega yupo katika ziara ya kushukuru kwa wananchi wake baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Mbunge Abdallah Ulega wa Jimbo la mkuranga akiwa sambamba na watendaji na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo akikagua mradi wa ufugaji wa samaki unaondeshwa na kikundi cha ufugaji samaki katika kijiji cha kibewa.Mh Ulega anaendelea na ziara zake za kushukuru wananchi wake.

Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega akimsikiliza Mganga wa Zahaniti ya Kijiji cha Sotele,Emily Bugingo kilichopo kata ya Dondo bara baada ya kutembelea Zahanati hiyo leo Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka,Globuya jamii)