Rais
Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa masikitiko makubwa
taarifa ya kifo cha aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Rais wa Pili wa Zanzibar Mheshimiwa Aboud Jumbe Mwinyi na Makamu
Mwenyekiti wa Kwanza wa CCM kilichotokea leo jijini Dar es Salaam.
Rais
Mstaafu amemuelezea Mzee Aboud Jumbe kama kiongozi mwenye mchango mkubwa katika
maendeleo na ustawi wa Zanzibar na mwenye mchango mkubwa katika uhai wa
Muungano wetu. Amesema, “Historia ya Chama cha Mapinduzi na ile ya
Muungano wetu haziwezi kukamilika bila kumtaja Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi”.
Rais
Mstaafu amewatumia salamu za rambirambi Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe
Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Dkt. Ali
Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa msiba
huu mkubwa katika taifa letu. Amesema:
“Naungana nanyi na familia ya marehemu, ndugu,
jamaa na wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kuomboleza msiba huu
mkubwa kwa Taifa letu. Mwenyezi Mungu na awape familia ya Marehemu moyo wa
subra na uvumilivu. Inna Lillahi Wainna Ilaihi Rajuun.”
Imetolewa
na:
Ofisi
ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne
Dar
es Salaam, 14 Agosti, 2016
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...