Rais wa klabu ya Simba, Evance Aveva.
Na Zainab Nyamka

KAMANDA  wa polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, ACP Chistopher Fuime amethibitisha kumshikilia rais wa klabu ya Simba, Evance Aveva, na alipoulizwa ni tuhuma gani zinazomkabili kiongozi huyo wa juu kabisa wa wekundu wa Msimbazi alisema ni vizuri swali hilo wakiulizwa TAKUKURU. Tumemshikilia toka juzi jioni na juhudi za kupatiwa dhamana zimeshindikana mpaka dakika hii kwani sisi kazi yetu ni kumshikilia tu ila mamlaka zaidi yapo TAKUKURU.

Aveva anashikiliwa na polisi kwa kibali cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU lakini bado haijafahamika moja kwa moja anakabiliwa na tuhuma gani huku baadhi ya watu wakidai ni matumizi mabaya ya fedha walizolipwa kutoka Etoile Du Sahel juu ya malipo ya Emanul Okwi pamoja na za Mbwana Samatta ambazo anadaiwa kuzihamisha kutoka kwenye akaunti ya klabu ya Simba.

“Kwa upande wangu siwezi kujua ila kwa maelezo zaidi  TAKUKURU wanaweza wakajua na ni lini huo uchunguzi  utakamilika na kumpeleka mahakamani. Sisi tunamshikilia kwasababu TAKUKURU hawana mahabusu binafsi,  na maswali yote  wangejibu sababu hasa ya kushikiliwa kwa Evance Aveva,” amesema Fuime 

Kwa upande wa TAKUKURU kupitia afisa habari Musa Misalaba amesema kuwa Aveva yupo kwenye mikono salama na wanamshikilia kwa uchunguzi, kwa sasa wanaendelea na uchunguzi kwani sheria inaturuhusu kufanya uchunguzi  na pia tunaruhusiwa kukamata, kupekuwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.

Sauti: Mahojiano kati ya Maulid Kitenge wa EFM Radio na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni pamoja na Msemaji wa TAKUKURU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...