Mkuu
wa mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Mrisho Gambo akiagana na Askofu wa Kanisa la
Anglikan Dayosisi ya Mount Kilimanjaro,Stanley Hotay(kulia) baada ya
mazungumzo yao.
|
Na Nteghenjwa Hosseah – Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo
ameendelea na ziara yake ya kujitambulisha kwa viongozi wa
dini ukiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kukutana na viongozi baada
ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hivi karibuni.
Mh.Gambo amekutana na Askofu wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT)Dayosisi ya Kaskazini Kati,Mchungaji
Solomon Masangwa , Askofu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies
of God(EAGT) mkoa wa Arusha,Leonard Mwizarubi na Askofu Stanley
Hotay wa Kanisa la Anglikana , Dayosisi ya Mount Kilimanjaro.
Katika mazungumzo na viongozi hao kwa nyakati
tofauti mbali na kujitambulisha aliwahakikisha dhamira ya serikali kulinda na
kuheshimu uhuru na haki ya kuabudu ambayo imekuwepo nchini kwa muda mrefu ikiwa
ni njia ya kuwa na taifa la watu wenye hofu ya Mungu.
Alisema kutokana na serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Rais Dr. John Joseph Magufuli kutaka kuwainua
wananchi wa chini kupitia mapato ya ndani halmashauri zimetenga asilimia
10 kutoka kwenye mapato hayo kwa ajili ya mikopo yenye riba nafuu kwa
Wanawake na Vijana wajasiriamali zitakazowawezesha kufanya shughuli
za uzalishaji mali.
Amewataka wawajulishe waumini wa dini
zote na serikali iko tayari kupanga utaratibu wa
maafisa maendeleo ya Jamii na Vijana kupita na
kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na madhehebu ya
dini hili iwe inufaishe watu wote katika mkoa huu bila kujali itikadi za kidini
wala kisiasa.
Askofu Stanley Hotay aliupongeza uongozi wa mkoa
kuimarisha hali ya utulivu na kuomba vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo Mkuu
wa mkoa ndiye Mwenyekiti wake kukabiliana na changamoto za kiusalama na
viashiria vya uvunjifu wa amani.
Aidha alishauri kutokana na idadi ya
watu wanaotumia usafiri wa anga kuongezeka kuna haja ya Serikali kufikiria
uwezekano wa kupanua zaidi uwanja wa ndege wa Arusha uliopo Kisongo ili
uweze kukidhi mahitaji ya sasa badala ya kutegemea uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Kilimanjaro(KIA) pekee.
Mh. Gambo amewahakikishia viongozi hao kuwa
serikali itakua ikiwashirikisha mipango mbalimbali inayokusudia kuitekeleza ili
watoe mawazo yao katika kuiboresha na kuifanya itekelezeke
kwa wepesi zaidi.
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...