Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa viwanja vya ubia kati ya UTT-PID na halmashauri ya manispaa ya Lindi uliofanyika katika ukumbi wa Kagwa, Lindi.
Mkuu wa mkoa akikabidhi hati kwa mmoja wa wanunuzi wa viwanja vya mradi.
Wageni mbalimbali walioalikwa ndani ya ukumbi wa Kagwa kuhudhuria uzinduzi huo.
Wageni mbalimbali walioalikwa ndani ya ukumbi wa Kagwa kuhudhuria uzinduzi huo. Mkuu wa mkoa wa Lindi amesifia utekelezaji wa mradi wa ubia wa viwanja kati ya Manispaa ya Lindi na Taasisi ya Miradi ya UTT- PID huku akizindua awamu ya pili ya utekelezaji ambapo itahusisha upimaji na uuzaji wa viwanja zaidi ya 8,000 katika maeneo tofauti ndani ya Manispaa ya Lindi. 

 Katika uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa katoliki wa Kagwa pia uliudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Meya wa Manispaa, Wakurugenzi wakuu wa Taasisi Mbalimbali, wawekezaji na wawakilishi kutoka Taasisi mbalimbali za Elimu ya juu. Uwasilishwaji wa maada juu utekelezaji wa awamu ya kwanza na mipango mikakati ya awamu ya pili ulifanyika kutoka pande zote mbili yaani UTT-PID and wataalamu toka Manispaa ya Lindi. Akieleza kwa kina Meneja Miradi wa Manispaa alisisitiza Taasisi Mbalimbali zilizonunua awamu ya kwanza kuanza ujenzi mara Moja huku akidai halmashauri imetenga zaidi ya ekari 1,500 bure kwa Chuo chochote kitachokua tayari kuanza kuwekeza ndani ya kipindi kifupi kijacho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...