Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza amefanya ziara ya kikazi Wilayani Mufindi yenye lengo la kukagua maendeleo ya miradi ya maji katika kijiji cha sawala kilichopo halmashauri ya Wiaya ya Mufindi pamoja na chanzo cha maji cha mjini Mafinga.

Akizungumza katika chanzo cha maji kilichopo kijiji cha sawala ,Mkuu wa Mkoa amewaagiza wahandisi wa maji kuhakikisha miundombinu ya mradi huo inakuwa mizuri kwa kufanya vitu vya kisasa zaidi pamoja na kuomba ushauri kutoka taasisi nyingine zilizoendelea zaidi katika sekta ya maji ili kuongeza ufanisi.

Akitoa taarifa ya mradi huo kwa Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi wa Wilaya ya Mufindi Dkt. Riziki Shemdoe amesema, mradi huo utajumuisha vijiji vinne ambavyo ni Sawala, Mtwango, Rufuna, na Ikangaga.

Aidha Dkt. Shemdoe amebainisha changamoto kubwa inayoukabili mradi huo kuwa ni uwezo mdogo wa kifedha kwa Mkandarasi jambo ambalo linasababisha ashindwe kukamilisha mradi kwa wakati .

Mradi huo ulianza kujengwa katika kijiji cha sawala mnamo mwezi wa 06 mwaka 2016 kwa lengo la kutoa huduma ya maji safi na salama, hadi kukamilika kwake utagharimu zaidi ya shilingi million 600 ikiwa ni fedha kutoka serikali kuu.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Dkt. Riziki Shemdoe mwenye kablasha mkononi akimuonesha,Mkuu wa Mkoa wa Iringa bomba ambalo linasafirisha maji 
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi Amina Masenza (katikati) mwenye ushungi, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William (kulia) wakitazama chanzo cha maji kijijini Sawala.
Msafara wa Mkuu wa Mkoa ukitazama ukuta uliojengwa kwenye chanzo cha maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...