NA VICTOR MASANGU, RUFIJI


Imefahamika kuwa nguvu kazi kubwa ya taifa inapotea bure kutokana na baadhi ya vijana wengine nchini Tanzania kuwa wavivu na kutojishughulisha na shughuli za kuleta maendeleo na badala yake wanaamua kujiingiza katika makundi ya uharifu,uvutaji wa madawa ya kulevya, pamoja na kupoteza muda mwingi kushinda kutwa nzima wakiwa wamekaa vijiweni bila kazi yoyote.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikiro wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa programu ya kambi ya vijana ya kuwafundisha masuala ya kilimo na maarifa ambayo ipo chini ya mamlaka ya uendelezaji wa bonde la mto rufiji (RUBADA) iliyofanyika katika kijiji cha Mkongo.

Ndikilo amebainishwa kwamb serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli isingependa kuona vijana wa kitanzania hawataki kutumia fursa zilizopo na kuamua kujiingiza katika vitendo ambavyo vipo kinyume kabisa na taratibu na sheria zilizowekwa ambapo wakati mwingine zinaweza kusababisha vurugu.

Naye mwakilishi wa shirika la chakula duniani (FAO) nchini Tanzania Fred Kafeero amesema kwamba kulingana na ripoti zinaonyesha asilimia 70 ya vijana katika africa hawana ajira hivyo kunahitajika juhudi za makusudi za kuweza kuwasaidia katika kilimo cha mboga mboga,huku Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Chwayo akiwaomba vijana hao kutumia fursa ya kilimo kupitia mafunzo watakayoyapata.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa ameutaka uongozi wa RUDABA kuhakikisha kwamba wanaepukana na malalamiko ambayo yalikuwa yanatolewa dhidi yao na badala yake waweke mikakati endelevu ya kuwasaidia vijana kujiendeleza zaidi pamoja na kuongeza juhudi za ujenzi wa viwanda kwa lengo la kuweza kuongeza kasi ya maendeleo na kukuza uchumi.

Kwa upande wao baadhi ya vijana ambao watanufaika na profamu hiyo akiwemo Saimoni Nyimmba pamoja na Joseph Bada wamesema kwamba mafunzo hayo ya kilimo na maarifa pindi watakapomaliza yataweza kuwasaidia kuwapatia kipato pamoja na kuachana na suala la kuwa tegemezi sambamba na kuondokana na kile kilimo cha kizamani.

MAFUNZO hayo ya kilimo na maarifa yataweza kuwanufaisha vijana wapatao 200 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania ambapo kwa sasa yataanza kuwanufaisha vijana 62 kutoka katika Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani ambapo ujuzi watakaupata wataweza kupata fursa ya kujiajiri wao wenyewe na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia sekta ya kilimo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...