THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

RC.MAKONDA KUJENGA MAKAO MAKUU YA BAKWATA KWA ZAIDI YA BILIONI TANO ,AKABIDHI RAMANI YA JENGO HILO JIJINI DAR LEO

⁠⁠⁠Na Bakari Issa Madjeshi, Globu ya Jamii 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekabidhi mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu kwa uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu nchini,BAKWATA ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya la Baraza hilo. 

Pamoja na kukabidhi ramani hiyo, Mkuu wa Mkoa huyo amesema jengo hilo litagharimu kiasi cha fedha 5, 080, 155, 600 ili kukamilika. Pia amesema jengo hilo mpaka kukamilika litakuwa la kipee na kupewa hadhi kama Taasisi kubwa ya Kiislamu na kusisitiza ujenzi wa jengo hilo hautazidi miezi 14.

Amesema amekabidhi mchoro huo kutokana na kutambua na kuthamini umuhimu wa BAKWATA katika Taifa pamoja na kuwataka Waislamu na wasiokuwa waislamu kujitokeza katika kutoa misaada hiyo. Pia ametoa shukrani kwa waislamu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kushereheka nao pamoja katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambapo amesema mwezi huo ndio uliokuwa chimbumbo la ujenzi wa jengo hilo la BAKWATA. 

Akitoa shukrani zake kwa Mkuu wa Mkoa huyo, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abuubakari Zuberi amewataka Waislamu kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa huyo ikiwa kuwataka kuamini ya kuwa na haki ya kupokea misaada kama Waislamu.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimuelekeza jambo Sheikh Mkuu wa Tanzania,Mufti,Abubakary Zubeir namna ujenzi wa ghorofa hilo utakavyokuwa,mara baada ya kukabidhiwa mchoro wa jengo hilo litakalogharimu zaidi bilioni tano,kulia ni Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , Alhaji Mussa Salum.PICHA NA MICHUZI JR. 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pampja na Sheikh Mkuu wa Tanzania,Mufti,Abubakary Zubeir wakitazama mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu,ambapo ujenzi wake utagharimu zaidi ya shilingi bilioni tano,ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya la Baraza hilo.
,kulia ni Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , Alhaji Mussa Salum .
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja naSheikh Mkuu wa Tanzania,Mufti wakionesha mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu kwa wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo fupi iliyofanyika jijini Dar mapema leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizaungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu kwa uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu nchini,BAKWATA ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya la Baraza hilo.
Sheikh Mkuu wa Tanzania,Mufti Abubakary Zubeir akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa,kabla ya kukabidhiwa mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu kwa uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu nchini,BAKWATA ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa jengo jipya la Baraza hilo.
 Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , Alhaji Mussa Salum akimkaribisha Sheikh Mkuu wa Tanzania,Mufti Abubakary Zubeir  mbele ya wageni waalikwa,kabla ya kukabidhiwa mchoro wa ramani wenye ghorofa tatu kwa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar ES Salaam,Mh Paul Makonda. 
 Baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia yalikuwa yakijiri kwenye hafla hiyo fupi. 
 Baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia yalikuwa yakijiri kwenye hafla hiyo fupi.


Hoja moja imeshachangiwa mpaka sasa.

  1. Anonymous Anasema:

    Napenda kuuliza tukianza kutumia pesa za umma kwa mambo kama haya je tupo tayari kuwajengea taasisi zote nyinginezo za dini??? Na hii bilioni 5 inatokea wapi??

    Huu ni mtazamo mwema tu kwa manufaa ya Taifa langu nalolipenda la Tanzania na sina niha mbaya na kama nimekosea ningeomba kuelimishwa. Ila kama zinatokea Serikalini (iwe kuu au ya mkoa) ipo wapi dhana ya Serikali kutokuwa na dini? Na ukianza jambo basi tujiandae kufanya mengineyo...