Shirika la ndege la RwandAir linategemea kupokea ndege mpya mbili aina ya Airbus zenye uwezo wa kubeba abiria 274 ifikapo mwezi Septemba 2016, ikiwa na Business class viti 30, Premium Economy Class viti 20 na Economy viti 224. Meneja mkazi wa Shirika hilo hapa nchini, Ibrahim Bukenya amesema ujio wa ndege hizo utaanzisha safari mpya za Bombay nchini India na Guangzhou nchini China. Aliendelea kusema kuwa Shirika hilo litaanzisha safari zake zingine kuelekea Abidjan, Harare, Durban, Abuja, Cotonou na Khartoum.
Meneja mkazi wa Shirika la ndege la RwandAir, Ibrahim Bukenya. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...