THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Safari Lager kuliteka soko na bia mpya ya kopo yenye ujazo wa 500ml

Bia ya kopo ya kwanza yenye ujazo wa mililita 500 kwa bia ya Kitanzania. 
 Kampuni ya Bia ya TBL kupitia bia yake ya Safari lager imezindua bia ya kopo ya kwanza yenye ujazo wa mililita 500 kwa bia ya Kitanzania. Akizungumza katika uzinduzi uliofanyika jijini Dar, Meneja Bidhaa wa Safari Lager, Edith Bebwa Nasuwa alisema “Ni bia ya kwanza ya Kitanzania ya kopo yenye ujazo wa mililita 500 ambayo italeta urahisi, unafuu na ladha nzuri ya aina yake kwa wapenzi wote wa bia ya Safari Lager” Bia hii ya kopo tayari imeshaanza kupatikana maeneo yote nchini kuanzia tarehe 26 Agosti 2016 na imeelezewa kuwa ni bia ya wajanja wenye kujiamini. 
“Bia mpya ya kopo ya Safari ni dhahiri kwamba imetengezwa kumpa umahiri Mtanzania katika safari ya maisha yake. Inapatikana kwa urahisi na kwa wakati muafaka hata wakati mtu anakwenda kwenye mihangaiko yake au kubeba akiwa anakwenda kwenye matembezi au safarini” alimalizia Edith Bebwa. 
Fuatilia kurasa za Safari Lager kupata habari zaidi 
 Bia ya kopo ya kwanza yenye ujazo wa mililita 500 kwa bia ya Kitanzania. 
Wadau wakifurahia bia ya kopo ya kwanza yenye ujazo wa mililita 500 kwa bia ya Kitanzania.